Katibu tawala wa
wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake.
Na Fredy Mgunda,Iringa
KATIBU tawala wa wilaya ya Iringa Joseph Chitinka amesema kuwa tarafa ya Isimani haina njaa kama ambavyo maneno
yanayozagaa mitaani kuwa ukanda wa ismani kuwa kuna njaa.
Akizungumza na blog hii Chitinka alisema kuwa kumekuwa na wanasiasa wanaoeneza kuwa tarafa ya Isimani
kuna njaa wakati hali halisi sio hiyo na kuongeza kuwa eneo hilo linachakula
cha kutosha na hakuna tatizo la njaa.
“Angalia mvua zinanyesha kwa
wingi na wananchi wamelima kwa wingi na mazao yanakuwa vizuri hivyo ismani
hakuna njaa na sijapokea taarifa yoyote ile ya kuwepo kwa njaa kwa kuwa
nimekuwa nikifanya ziara katika maeneo hayo mara kwa mara na nimejihakikishia
kuwa hakuina njaa hali ya chakula ni nzuri na kuwaomba wananchi kuacha
kuwasikiliza wanasiasa”.alisema Chitinka
Chitinka aliwataka wananchi
kuacha kutumia mazao ya mahindi,mtama na uwele kupikia pombe kwa kuwa kufanya
hivyo kutapunguza uwepo wa chakula katika eneo hilo.
Unakuta mtu anashawishiwa
kuuza mahindi kwa mpika pombe wakatyi anajua kuwa hana chakula cha kutosha
nasema ni marufuku kwa wananchi kupika pombe kwa kutumia mahindi,uwele na mtama
ili kuendelea kutunza chakula hicho.
Aidha Chitinka alisema kuwa
sasa ni fursa kwa wafanyabiasha kuuza mahindi katika maeneo mbalimba ya wilaya
ya iringa kwa kuwa bei ya mahindi kwa sasa ni nzuri.
Hivi hawa wanansiasa
wanayatoa wapi maneno ya uongo kuwa ismani kuna njaa naomba waje na takwimu na
sio kuposha wananchi serikali ndio inaweza kutangaza kama sehemu kuna njaa na
sio mtu mwingine yoyote.
“Serikali ndio chombo cha
mwisho kuthibitisha kuwa Isimani kuna njaa sio kila mtu anaweza kuongelea mambo
ya serikali naomba hawa wanansiasa waache mara moja kupotosha wananchi na
wakiendelea kupotosha jamii tutawachukulia hatua za kisheria maana hatuna
tatizo la chakula katika tarafa ya ismani”.alisema Chitinka
0 comments:
Post a Comment