Katibu wa Halmashauri kuu ya taifa (NEC) Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Humphrey Polepole amewataka watumishi wa Halmashuri zote nchini kufanya kazi kwa kufuata mwongozo kutoka kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020.
Maagizo hayo ameyatoa leo katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Kibamba CCM.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake katika Manispaa za jijini la Dar es Salaam na hatimaye Halmashauri zote nchini.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Ndg. Pole alisema watumishi wafanye kazi kwa weledi na kwa kufuata kilichoandikwa ndani ya ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020.
```"Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi inatoa mwongozo wa vitu vya kufanya kwa ajili ya kuleta maendeleo katika nchi yetu, watumishi nawasihi kufanya kwa kufuata ilani hiyo" alisema Polepole na kuendelea;-
"Tuwajibike kwa wananchi kwani bila wao msingekuwa watumishi wa umma naomba mfanye kazi kwa weledi mkubwa na kuzingatia utu kwani binadamu wote ni sawa"``` alisema Polepole.
Pia akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Matiku Makori alisema wameyapokea yote aliyozungumza Ndg. Polepole na kuahidi kufanya kazi kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020.
```"Nakushuru sana kwa kuweza kuja hapa kwa pamoja tunakuahidi kutekeleza yote uliyotuagiza na pia tutafanya kazi kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015-2020"``` alisema Mh. Kisare Makori.
```Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo```.
0 comments:
Post a Comment