Tuesday, April 10, 2018

CCM MANISPAA YA IRINGA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI TANO KUTATUA BAADHI YA CHANGAMOTO KATIKA HOSPITAL YA FRELIMO

 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa (CCM) Said Rubeya akikambizi vifaa kwa ajili ya kutatua baadhi ya changamoto kwa kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000) ili kuboresha maisha ya wananchi wanaohudumiwa na hospital hiyo
 Baadhi ya wananchi,makada wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa na viongozi wa chama hicho waliokuwa wameudhulia makabidhiano ya vifaa kati ya uongozi wa hospital na viongozi wa chama hicho manispaa ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA cha mapinduzi manispaa ya Iringa kimetumia zaidi ya shilingi million tano kuanza kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili hospitali ya Frelimo iliyopo wilaya ya Iringa kwa kununua mashine mbili za kufulia na televisheni moja aina ya LG nchi 43.

Akizungumza wakati wa kukatibidhi vifaa hivyo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi hivyo wameamua kuanza kuzitatua kwa awamu na kuangalia vipaumbele stahili.

“Tulikuja kwenye ziara hapa na viongozi wangu na tulikutana na viongozi wa hospatali hii wakatueleza changamoto nyingi sana ambazo ni ngumu kutekeleza kwa siku moja hivyo tulitoka na vipaumbele vyetu sisi kama chama ndio maana leo tumenza na hili na tutafuta na jingine” alisema Rubeya

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi mganga mfawidhi wa hospital hiyo, Dr Pilila Zambi alisema kuwa hospital hiyo inakabiliwa na changamoto zifuatazo jengo la vipimo na uchunguzi,wodi ya kulaza wagonjwa,wodi ya watoto,wodi ya kulaza wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza,jengo la utakasaji wa vifaa,jengo la kufulia nguo,nyumba za watumishi na ukosefu wa uzio.

Aidha Dr Zambi aliongeza kuwa hospital hiyo inaupungufu wa vifaa tiba ambavyo vimekuwa vikikamisha shughuli za kutoa huduma bora kwa wananchi,vifaa hivyo ni biochemistry machine,hematology machine Viral load analyser,Ultrasound machine na X-ray machine.

“Tukipata pia mashine kama mashine ya utakasaji, mashine ya kufulia na automatic genereta basi hapo tutakuwa tumefanikiwa kutatua changamoto za hospitali na tutatoa huduma bora kwa wananchi wanakuja kupata huduma katika hospital hii” alisema Zambi

Rubeya alisema kuwa kutokana na changamoto hizo ndio maana wameanza na kununua mashine mbili za umeme za kufulia nguo zenye thamani ya shilingi milioni tatu (3,000,000) na televisheni moja aina ya LG nchi 43 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki mbili (2,200,000)

“Tuliona tuanze na vifaa hivi vidogo kwasababu inasikitisha kuona kuwa nguo chafu zenye vimelea vya magonjwa mbalimbali vinapitishwa katika ya mji hadi hospital ya Rufaa hivyo tukaamua kutatua kwa hii changamoto, pia wauguzi na madaktari mnatakiwa kujua nini kinaendelea nchi kwetu na nje ya nchi hiyo tukaamua kuwaletea TV hii kwa ajili ya mafunzo mbalimbali” alisema Rubeya

akizungumza kwa niaba ya mstahiki  meya diwani wa kata ya mivinjeni Frank Nyalusi amewataka viongozi wote kuleta maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa  na kuwashukulu viongozi wa chama cha mapinduzi kwa kuwafungulia njia ya maendeleo.

“Mimi binafsi niwapongezee chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa mliyoifanya hapa kwa kutusaidia kutatua changamoto za hospital hii” alisema Nyalusi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More