Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati anasherekea sikuku ya pasaka na watoto yatima wa kituo cha Huruma center kilichopo Kigamboni Donbosco
Jamii bado inauelewa
mdogo katika utunzaji wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuamini
kuwa suala hilo ni jukumu la wafadhili kutoka nchi nyingine.
Mchungaji Joyce Gandango
msimamizi wa kituo cha Huruma Center ameeleza hayo mbele ya mbunge wa viti
maalumu mkoa wa Iringa Mh Ritta Kbati alipokuwa akishiriki chakula cha mchana
na watoto katika kituo hicho kwenye sikukuu ya pasaka.
Msimamizi huyo ameeleza
kuwa bado jamii haina muamuko katika kujitokeza kutunza watoto wa vituoni kwa
kuamini kuwa wadhamini hutoa kila kitu.
Amezitaja changamoto nyingine zinazowakabili katika
kituo hicho ni ufinyu wa bajeti kutokana na wahisani kuanza kuondoka pamoja na
kituo kushindwa kujitegemea na kujiendesha chenyewe.
Kwa upande wake mbunge
wa viti maalumu Mh,Ritta Kabati ameahidi kushirikiana na viongozi wa kituo
hicho katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuzifikisha bungeni ili
serikali iweze kuona namna ya itakavyowasaidia kuzitatua.
0 comments:
Post a Comment