Wednesday, April 5, 2017

TANZANITE ONE KUJENGA UPYA SHULE YENYE MADARASA MANNE NA WANAFUNZI 1126 ANDREA NGOBOLE

Mkurugenzi mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma pamoja na viongozi wa serikali na wajumbe  wa kamati ya shule ya Songambele  akikagua madarasa ambayo hayatumiki  kutokana na nyufa baada ya shule kukumbwa na mafuriko na kutangaza kujenga madarasa  saba.




Mkurugenzi mwenza wa Tanzanite One,Faisal Juma akizungumza katika mkutano na wazazi wa shule ya msingi Songambele  ambayo ina uhaba wa madarasa na kutangaza kujenga madarasa  saba Mwaka huu ili kupunguza tabu waipatayo wanafunzi hao kwa kukoisa vyumba vya madarasa.

ANDREA NGOBOLE; PMT
Siku tatu baada ya kuripotiwa shule ya msingi Songambele iliyopo Mererani wilaya ya Simanjiro, yenye wanafunzi 1126 kusoma katika madarasa manne,Kampuni ya Tanzanite One imetangaza kujenga madarasa saba ili kuondoa uhaba wa madarasa katika shule hiyo.

Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya Tanzanite One,Faisal Shabhai amesema,baada ya kuona kwenye vyombo vya habari shida ya madarasa katika shule hiyo,wameamua kujitokeza kujenga shule hiyo.

Shabhai alisema,Tanzanite one kama mwekezaji Katika migodi ya Tanzanite wanawajibu wa kusaidia masuala ya kijamii hasa kwa kuwa wananufaika na madini ya Tanzanite.

"Tunajua tunawajibu wa kusaidia jamii hivyo tutajenga madarasa  saba katika shule hii"alisema

Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro,Zuwena Omar  alishukuru kampuni Tanzanite One kwa msaada waliotoa kujenga madarasa hayo.

Omar alitoa wito kwa wawekezaji wengine waliopo Mererani kusaidia maendeleo ya Mererani.

Mwalimu Mkuu shule hiyo.Mwanahamisi Mussa alisema wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa madarasa, matundu 40 ya vyoo,Nyumba za walimu na ofisi kwani wanafanyakazi chini ya miti.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More