Halmashauri
ya jiji la Arusha imeahidi kutoa shilingi laki saba na ishiri kupitia mfuko wa afya ya jamii (TIKA) kwa watu
wenye ulemavu kwaajili ya kuwalipia huduma za afya bure ndani ya mwaka mmoja kwa
vituo vyote vilivyopo ndani ya jiji la hilo
Akizungumza katika mkutano ulIowakutanisha watu
wenye ulemavu na uongozi wa halmashauri ya jiji la arusha mkurugenzi mtendaji wa jiji
la Arusha Ndg Athumani Juma Kihamia amesema kuwa lengo la kuwapatia fedha hizo
kutokana na walemavu wengi ambao wamekuwa wakiosamitaji ya kufanyia kazi hali
inayopelekea kundi hilo kuwa masikini.
Kwa upande wake mratibu wa mfuko wa afya ya jamii TIKA
Bi Rossemary Tigando ameelezea mipango yao ambayo ni pamoja na kuhakikisha watu
wote wenye ulemavu kupata huduma ya afya ndani ya mwaka mmoja bila usumbufu wowote katika hospitali zote za
halmashauri jiji la arusha.
Aidha watu wenye ulemavu wamepongeza hatua hiyo
iliyochukuliwa na uongozi wa halmashauri na kutoa wito kwa wenzao kufuata
taratibu zilizotolewa za usajili wa kadi ya bima ili isilete adha kwa watoa
huduma
Pamoja na kuisifia hatua hiyo kutoka kwa halmashauri
watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja
na,mitaji,vifaa vya kujimudu kama miguu mikono bandia,mikopo yenye riba
nafuu,kutokuwa na miundombinu rafiki na mengine mengi waliorodhesha kwenye
risala yao kwa mgeni rasmi.
0 comments:
Post a Comment