Tuesday, April 25, 2017

FORM ZA USAJILI WA RITTA KABATI CHALLENGE CUP ZATOLEWA RASMI

Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo Gerald malekela akitangaza rasmi kuanza kuchukuliwa kwa form za usijili mbele ya waandishi wa habari.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mashindano ya Mpira wa miguu ya Ritta Kabati challenge cup yanatarajiwa kuanza hivi Karibuni baada ya Leo Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo Gerald malekela kutangaza rasmi kuanza kuchukuliwa kwa form za usijili.

Akizungumza na waandishi wa habari Gerald malekela alisema kuwa lengo la mshindano ya Ritta Kabati challenge cup ni kuinua vipaji mbalimbali ambavyo vilikuwa vimekosa fursa ya kuvionyesha kutokana na kutokuwa na mashindano ya Mara kwa Mara.

"Tumeamua kuanzisha Mashindano haya ili mpira wa miguu mkoa wa Iringa uchezwe kila wakati na tusisubili tu mashindano yanayo andaliwa na vyama vya mpira Mkoani iringa wakati wadau wa kuanzisha Mashindano tu na tunauwezo huo"alisema Malekela

Katika hatua nyingine Malekela alizitaja zawadi za washindi watatu wa juu wa Mashindano hayo kuwa ni mshindi wa kwanza atapaata pikipiki moja maarufu kama bodaboda,jezi jozi moja pamoja na kombe ,mshindi wa pili atajinyakulia Pesa taslim shilingi lakini tano na jozi moja ya jezi na mshindi wa tatu atajinyakulia Pesa taslimu shilingi lakini mbili na nusu pamoja na jozi moja ya jezi hizo ni Zawadi kwa upande wa timu lakini kutakuwa zawadi za mchezaji bora wa Mashindano atajinyakulia shilingi elfu hamsini,mfungaji bora atajinyakulia elfu hamsini na kikundi bora cha ushangiliaji kitajinyakulia shilingi lakini moja.

Aidha Malekela alisema kuwa Mashindano hayo yatakuwa na kiingilio cha shilingi elfu ishirini kwa kuwa ni Mashindano makubwa lazima yawe na kiingilio.

"Hata kwenye kombe la mbuzi tu kuna kiingilio hivyo hata huku tumeweka kiingilio ili kuyapa ubora Mashindano na ukisema hakuna kiingilio kutakuwa na vulugu ya timu kutaka kushiriki kwenye Mashindano hivyo kwa kuwa Mashindano yatakuwa ya ukubwa wa aina yake hivyo ni lazima timu ziingilie kiingilio" Alisema Malekela

Malekela alisema kuwa kwa anazikaribisha timu zote za mkoa wa Iringa kwa ujumla na kuwaambia kuwa hakutakuwa na masharti ya kusajili wachezaji kwa kuwa Mashindano haya yameipa uhuru timu kusajili wachezaji kutokana na uwezo wao hata wakisajili wachezaji kutokana ligi kuu ya Tanzania ni uwezo wao.

"Tunazikaribisha timu kusajili hata wachezaji wa ligi kuu kama wakina kichuya,msuva,ngoma ,kamsoko,ndemla na wachezaji wengine bora mradi wanafuata vigezo na masharti ya Mashindano lengo letu mpira uchezwe Mkoani iringa na wapenzi wa mpira wa miguu kupata mahali pa kwanza kufurahi kuona vijana wakisakata kabumbu katika viwanja mbalimbali ndani ya mkoa wa Iringa "alisema Malekela

Lakini Malekela alisema kuwa form za usajili wa timu zitachukuliwa ndani ya siku saba tu baada ya hapo itakuwa ni vikao vya mwisho kwa ajili ya kuanzia Mashindano na form zitabatikan pale Nuru FM na country fm au unaweza kumtafuta Fredy Mgunda kwa namba hii 0714 201006 na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushuhudia Mashindano hayo ambayo yataendeshwa kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia kuwa na waamulizi bora.

Mashindano haya tumeyaanzisha kwa kushikiana na chama cha Mpira Mkoani iringa hivyo tunaamini Mashindano yatakuwa bora sana na kutoa burudani kwa wapenzi wa mpira Mkoani hapa.

Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati alisema kuwa Mashindano hayo nataka yawe mfano Mkoani hapa kwa kuwa yanazawadi kubwa na yatakuwa bora kwa kuwa tupo pamoja na chama cha Mpira Mkoani hapa.

"Mimi niombe timu zijitokeze kwa wingi kushiriki Mashindano haya na vijana wetu kuonyesha vipaji vyao ambayo vitatusaidia kuzisaidia timu zetu kupata wachezaji wazuri kwa hiyo naomba wadau kujitokeza kuangalia na kutoa maoni yao ili tuweze kuondoa mapungufu yanayojitokeza"alisema Kabati

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More