Wednesday, April 5, 2017

MBOWE ATANGAZA KWENDA MAHAKAMANI

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamewachagua wajumbe 7 wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania huku wagombea wawili wa CHADEMA wakipigiwa kura za 'HAPANA' na hivyo kushindwa kupitishwa.
Wabunge  hao wa CHADEMA ni Lawrence Masha na Ezekiel Wenje, ambao pia waliungana na wagombea wengine wote kujieleza mbele ya wabunge kabla ya zoezi la upigaji kura.

Kwa upande wa CCM, walioshinda ni
1. Fancy Nkuhi
2. Happiness Legiko
3. Maryam Ussi Yahya
4. Dkt Abdullah Makame
5. Dkt Ngwaru Maghembe
6. Alhaj Adam Kimbisa

CUF iliyokuwa na wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo
Awali palitokea mabishano ya kikanuni juu ya wagombea wa CHADEMA yaliyosabaishwa na chama hicho kuweka wagombea wawili pekee wakati nafasi kwa ajili ya chama hicho zikiwa mbili pia.

Baadhi ya wabunge walitaka Spika atumie utaratibu wa kuwahoji wabunge kama wnawakubali ama lah, huku wabunge wa CHADEMA wakitaka wagombea hao wapigiwe kura sawa na wengine, ambapo wapiga kura wangelazimika kupiga kura za kuwakubali wagombea hao hata kama hawawataki.

Baada ya mvutano wa takriban saa moja, Spika Job Ndugai aliamua kura zipigwe, lakini kwa kundi la wagombea wa CHADEMA akaelekeza kuwa wapiga kura wa uhuru wa kuweka alama ya 'tick' kama wanamkubali mgombea au alama ya 'X' kama hawamkubali.

"Sasa maelekezo yangu ni kwamba ukifika kwa wagombea wa Chadema weka X kama humtaki, na weka tick kama unamtaka" Alihitimisha Ndugai

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo majira ya saa 7 usiku, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema haki haikutendeka ikiwa ni pamoja na ubabe kutumika na upindishwaji wa kanuni, hivyo watakwenda kuitafuta haki yao mahakamani.

Hawa ndiyo walikuwa wagombea kwa upande wa CCM

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More