Wednesday, April 26, 2017

BUNGE SC YAILAZA BARAZA LA WAWAKILISHI 4-0.

Timu ya Bunge Sports imeichakaza timu ya Baraza la Wawakilishi mabao 4-0 ,katika mchezo wa kusisimua uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Katika mchezo huo uliochezwa kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania, Bunge Sports ilipata mabao mawili kila kipindi.

Bao la kwanza lilifungwa na Cosato Chumi 'Gaza' baada ya kupokea pasi ya Mwigulu Nchemba katika dakika ya 13 ya mchezo.

Sixtus Mapunda aliandikia Bunge bao la pili dakika ya 25 kufuatia pasi ya Godfrey Mgimwa 'Neymar' .
Mpaka mapumziko Bunge SC ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili Bunge ilianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu kwa njia penati iliyofungwa na Mohamed Mchengerwa kufuatia rafu aliyochezewa Chumi aliyekuwa anaenda kuliona lango la Baraza la Wawakilishi.

Bao la nne lilifungwa na Flatey Maseyi dakika ya mwisho ya mchezo baada ya Omary King kumtangulizia pande la ndani ya Box.

Kwa upande wa netball Bunge Queens iliwashinda Wawakilishi magoli 43 -14

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More