NA
MWANDISHI WETU, KOROGWE.
BONANZA
la Michezo la siku sita litakalohusisha walimu wa michezo na wadau mbalimbali
linatarajiwa kufanyika Mei 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Halmashauri ya
Korogwe .
Bonanza
hilo limefadhiliwa na asasi ya Inuka wenye lengo la kupiga vita madawa ya
kulevya na kuhamasisha michezo na nidhamu kwa jamii
Akizungumza
na waandishi wa habari leo,Kaimu Mratibu wa Inuka Kanda ya Ziwa,Gaudance Msuya
alisema lengo kubwa litakuwa kuiamsha jamii na kupenda kushiriki kwenye michezo
ili kuimarisha afya zao.
Alisema
katika bonanza hilo michezo itakayokuwepo ni mpira wa miguu,riadhaa ,mpira wa
pete,kuvuta
kamba na kukimbiza kuku
na kutembea na
magunia.
Aidha
alisema washindi kwenye michezo hiyo wata zawadiwa zawadi mbalimbali ambapo
zaidi ya milioni mbili zimetengwa kwa ajili ya zawadi kwa washiriki watakofanya
vizuri.
“Ndugu
zangu watu wa Korogwe hii ni fursa ya kipekee hivyo ninawaomba mjitokeze kwa
wingi kushiriki kwenye bonanza hili ambalo litakuwa na faida kubwa licha ya
kuwepo kwa zawadi hizo”Alisema.
Hata
hivyo alisema kwa washiriki ambao wangependa kushiriki wawasiliane na Ofisa
Michezo wilaya ya Korogwe ili kuweza kuthibitisha ushiriki
wao.
Mratibu
huyo aliyataka mashirika mbalimbali ikiwemo mabenki kuona namna ya kuunga mkono
jambo hilo kwa kuona namna ya kufadhili ambapo wanaweza kuwasiliana na mratibu
huyo kwa simu namna 0683122320/0683122340.
0 comments:
Post a Comment