MBUNGE
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT- Wazalendo) ameitaka serikali
kumwagiza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kubaini
wizi wa Sh. 608 trilioni zilizokopwa kupitia Benki ya Stanbic yenye tawi
lake nchini hapa.
Alitoa kauli hiyo jana
bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kutaka kujua ni hatua gani
ambazo zinachukuliwa kutokana na ufisadi mkubwa wa fedha hizo ambazo ni
trilioni 6.8.
“Jumla
ya fedha ambazo serikali ilizikopa nje kwa mfumo wa namna hiyo ni
shilingi trilioni 6.8 na katika taarifa ya hukumu inaonesha mtindo huo
wa kutumia vikampuni kwa ajili ya kupata mikopo imekuwa ikitumika na
mabenki mengi ya kibiashara hapa nchini.
“Serikali
haioni kwamba umefika wakati CAG aweze kufanya ukaguzi maalum wa mikopo
yote ya kibiashara ambayo serikali imechukua katika kipindi hicho ili
kuweza kujua kama pia kulikuwa kuna aina za rushwa za namna hiyo ambazo
zimekuwa zinafanyika,”alihoji Zitto.
Zitto alisema
DFA (Hukumu ya Uingereza) ilikuwa ina lengo la kuilinda Benk ya
Uingereza ambayo ndiyo ilitoa hongo kwa maofisa wa Tanzania ili iweze
kupata biashara ambapo alihoji, serikali haioni kwamba ni wakati muafaka
sasa kufungua kesi dhidi ya benki hiyo ya Uingereza ili iwe fundisho
kwa kampuni za nje zinazohonga kwa lengo la kupata biashara katika nchi
za kiafrika
Akijibu maswali hayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji George Masaju alisema
CAG anayo majukumu ya kikatiba na hilo ni jukumu ambalo anaweza
kulitekeleza wakati wowote ili kujiridhisha kama mikopo hiyo ambayo
imekuwa ikipatikana kwa namna ambayo inaifanya nchi iingie kwenye
hasara.
Alisema,
kama Zitto anazo taarifa zozote zinazoweza kuisaidia serikali ama
kufungua shauti la madai ama jinai ashirikiane na vyombo husika ikiwemo
Ofisi ya AG na kuliangalia ili kuona kama linakidhi sifa na sheria na
kwa kuzingatia pia uhusiano uliopo kwa nchi ya Uingereza ili kuona kama
kesi ya jinai inaweza kufunguliwa.
Aidha alisema
serikali imepokea ushauri wa Zitto na itaufanyia kazi kwa kuzingatia
sheria za ndani ya nchi na uhusiano wa kisheria katika Jumuiya ya
Kimataifa.
Awali katika swali la msingi la Zitto alitaka kujua serikali inaichukulia hatua gani Stanbic Bank ili walipe fidia zaidi.
“Mwaka
2013 serikali ilizuia hatifungani ya thamani ya dola za Kimarekani
milioni 600 (USD 600.0 mili) kupitia Benki ya Sdandard yenye tawi hapa
nchini (Stabic).
“Shirika
la Corrupition Watch la Uingereza kwa kutumia vyombo kama IFM imeonesha
kuwa hatifungani hiyo imeipa Serikali ya Tanziania hasara ya Dola za
Marekani miliono 80 na serikali imelipwa fidia Dola za Marekani milioni
6.
“Je kwa nini serikali haichukulii hatua Stanbic Bank ili ilipe fidia zaidi?”alihoji Zitto.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashantu Kijaju alisema,
serikali imefuatilia taarifa za hasara kwa Serikali ya Tanzania ya Dola
za Marekani 80 iliyotajwa na Zitto lakini haikupata ushahidi wake.
0 comments:
Post a Comment