Thursday, February 11, 2016

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU IRINGA (IRFA) KUJENGA UWANJA WA KISASA

 
kulia  ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu  mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na baadhi ya viongozi wa uwanja wa samora.

NA RAYMOND MINJA IRINGA

Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) kiko mbioni kujenga uwanja wake wa kisasa utakaosaidia kuendeshea ligi mbalimbali zikiwemo ligi za kimataifa  hali itakayosaidia  kuinua soka la mkoa huo .


Akizungumza ofisini kwake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu  mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava alisema wameamua kujenga uwanja wao  ili kuepukana na adha wanayopata kutokana na kukosa sehemu ya kuendeshea ligi  mbalimbali .


Alisema tayari wameshapata eneo la hekari 14 katika eneo la kitwiru ndani ya manispaa ya Iringa  na sasa kinachosubiriwa ni kumaliza mazungumzo kati ya chama hicho na manispa ya Iringa ili kuweza kumilikishwa eneo hilo ili liwe mali yao kabisa tofauti na apo awali ambao manispaa hiyo ilikuwa inataka kuingia nao ubia


“Tayari hili swala liko katika hatua za mwisho na tayari tumesha fanya mazungumzo tunataka  tujenge  uwanja wetu wenyewe wa kisasa ambao tunaweza kucheza mechi za kimataifa  kwani tumekuwa tukipata tabu ya viwanja vya kuchezea na hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuuwa soka la mkoa wetu ”alisema Kuyava


Alisema wanasubiri majibu ya maombi waliyopeleka katika manispaa hiyo ili kuweza kupunguziwa bei li kuanza mchakato wa kulipa fidia kwa wamiliki wa maeneo hayo ili waanze mchakato wa uwanja huo wa kisasa .


Alisema kuwa mara nyingi timu zimekuwa hazi pati kitu  wanapotumia viwanja vya watu  kwani asilimia 16 za mapato yanayopatikana kutokana na kingilio huchukuliwa na wamilika  wa kiwanja na asilimia ndogo inabaki ndio zinagawanywa katika maeno mengine na kujikuta timu hazinufaiki na chochote .


Alisema kuwa hapo awali walikuwa wakitumia uwanja wa samora ambao bado uko katika matengenezo tena ya kusuasu kwa kuwa mpaka sasa bado wanadai kusubiri nyasi za kupanda jambo litakalorudisha michezo nyuma endapo hawatakuwa na maono ya kuwa na kiwanja chao wenyewe .


Kwa upande wa wadau wa soka mkoa wa Iringa Ally salehe ambaye pia ni shabiki wa timu ya lipuli anasema kuwa endapo juhudi za makusudi zitafanyika na kufanikisha ujenzi wa uwanja huo basi ni dhahiri kuwa soka la mkoa wa iringa litapanda  kwa kiasi kikubwa .


Alisema kuwa katika mkoa wa Iringa kuna vipaji vingi vya michezo  ikiwemo wachezaji wa mpira wa miguu lakini wamekuwa wakikosa sehemu za kufanyia mazoezi ili kukuza vipaji vyao  hivyo kujengwa kwa uwanja huo wa kisasa utafungua fursa za ajira kwa vijana wengi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More