Mwenyekiti
wa Chama cha Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda (pichani), amewataharisha
wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa makini wawapo barabarani, ili kuepukana na
vitendo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu
kwa kutumia pikipiki.
Kayanda alitoa tahadhari hiyo jana Jijini Mwanza baada ya kupokea
malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya ukwapuaji vinavyofanywa na baadhi ya
watu wanaojifanya waendesha pikipiki, jambo linalochafua taswira ya waendesha
pikipiki Mkoani Mwanza.
Tayari watu kadha wamefikisha malalamiko yao kwa uongozi wa bodaboda Mkoani Mwanza, baada ya kukumbwa na
kadhia ya kukwapuliwa mikoba pamoja na mabegi yao, ambapo mmoja wa wahanga wa
matukio hayo Diana Abdallah ameeleza kukwapuliwa mkoba wake uliokuwa na pesa
pamoja na vito vya thamani wakati akitokwa kwenye shughuli zake.
"Nilikuwa maeneo ya Nyegezi ambapo nilikuwa nikitoka kwenye shughuli zangu, nilikwapuliwa mkoba wangu ambao ulikuwa na pesa shilingi Laki Nane, Simu ya shilingi Laki mbili na nusu, Pete sita za Silver zenye thamani ya shili laki moja na elfu ishiri na sita pamoja na miwani ya macho ya shilingi Laki nne. Watuhumiwa waliweza kukamatwa na kesi iko polisi katika kituo cha Igogo".Alisema Abdallah
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita matumizi ya
dawa za kulevya na uhalifu nchini Edwin Soko, analaani Vitendo hivyo vya
ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi ya watu kwa kutumia bodaboda ambavyo vimekuwa
vikiwakumba watembea kwa miguu Jijini Mwanza, ambapo ameomba jeshi la polisi
kutoa ushirikiano wake kwa ajili ya kuvikomesha.
0 comments:
Post a Comment