Wednesday, February 17, 2016

KATIBU WA CWT MANISPAA YA IRINGA AMETANGAZA MGOGORO NA MKURUNGEZI WA MANISPAA YA IRINGA

 katibu wa cha walimu manispaa ya iringa mwalimu Fortunate Njalali akiwa ofisini kwake


siku kadhaa zimepita toka kufanyike uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la manispaa ya iringa kwa ajiri ya kujadili baadhi ya agenda za kulijenga upya baraza hilo,lakini chama cha walimu manispaa ya iringa kimegoma kuhudhuria baraza hilo kutokana na kukiuka baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali.

Akizungumza na blog hii katibu wa cha walimu manispaa ya iringa mwalimu Fortunate Njalali amesema kuwa sababu ya kugoma kuingia kwenye baraza  la halmashauri ya manispaa ya iringa kwa kuwa baraza hilo limepitwa na muda hivyo kunaitajika kuliunda baraza jimpya ndio waweze kuingia kwenye baraza la wafanyakazi.

Aidha katibu Njalali amesema kuwa wamekuwa wakiingia kwenye baraza la wafanyakazi kinyume cha sheria kwa majadiliano maalumu hivyo walikuwa wakihudhuria baraza batili na walikuwa wakimuambia mkurungezi juu ya swala hilo.

Njalali amesema kuwa haiwezekani baraza la wafanyakazi likawa na viongozi wengi kuliko wafanyakazi wenyewe hivyo watakuwa hawawatendei haki kwa kuwa hawatakuwa na hoja za msingi zinazowahusu wafanyakazi wenyewe.

“Angalia humu kwenye baraza hili tumejaa viongozi tu watumishe au walimu wenyewe wanawakilishwa na nani na tutengemee matokeo gani kwa miaka ya baadae kwa kupitisha bajeti isiyokuwa na mashiko kwa wahusika”.alisema Njalali

Njalali ameongeza kuwa hawawezi kuingia kwenye baraza la wafanyakazi ambalo halina viongozi kwa kuwa viongozi waliopo hawana uwezo wa kuwa viongozi wa kuongoza baraza hilo kutokana na uwezo wao wa kitendaji.

“Hatuwezi kuongozwa na wajumbe na viongozi haramu kwa kuwa wamekiuka sheria  na wanaijua hilo na kama mkurugenzi atandesha baraza hilo basi baraza hilo litakuwa batili kwa kuwa chama cha walimu ndio waliosaini mkataba huo”.alisema Njalali

Lakini Njalalia ametangaza rasmi mgogoro na mkurungezi wa manispaa ya iringa kwa kukiuka makubaliona waliokubaliana hapo awali wakati wa kusaini mkataba na kuwahidi walimu kuwa watampeleka mkurugezi CMA

“Nimemwandikia barua kuwa nimetangaza mgogoro na mkurugezi na nimempa siku tano kukutana na viongozi wa chama cha walimu manispaa ya iringa vinginevyo tarehe kumi na sita mwezi huu nampeleka kwenye baraza la usuruhishi CMA kwa kukiuka sheria na makubailiona ya mkataba wetu”.alisema Njalali

Njalali alimalizia kwa kusema kuwa baraza la wafanyakazi linafaida kwa watumishi kwa kuwa wanajadiliana na muaji wao juu ya mazingira ya kazi yao na wafanya nini ili kuboresha ufanyaji wa kazi zao na kuongeza ubunifu wa kuboresha kazi.

“Tumekuwa tunapitisha bajeti nyingi lakini hakuna mrejesho wowote ule wa ile bajeti tunayoipitisha  hivyo tumekuwa tunaburuzwa mara kwa mara kwa sasa basi hatutaki kuburuzwa tena tunataka haki yetu na ndio maana tumetangaza mgogoro na mkurugenzi wa manispaa ya iringa”alisema Njalali.

Tulipomtafuta mkurugezi wa manispaa ya iringa hakupatika kujibia kero hii iliyotolewa na katibu wa CWT,hata hivyo baraza la wafanyakazi lilifanyika na wakafanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More