Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove akiwa askofu mkuu wa kanisa la Orthodox Tanzania Dimitrios Zachalegas
picha baadhi ya vongozi waliokuwa wamehudhuria katika eneo hilo la kuweka jiwe la msingi la shule itakayojengwa kwa ufadhili wa kanisa la Orthodox
Na Esta Malibiche Majira
Iringa
Diwani wa kata ya Nduli Basher mtove amewashukuru wafadhiri kutoka kanisa la Orthodox kwa
kujitolea kujenga shule ya sekondari
pamoja na maabara,na kuwataka waendelee kuisaidia serikali bila kuchoka.
Alisema baada ya kuona
adha kubwa kutembea kwa umbali
zaidi ya kilomitre 7 kwenda kupata elimu ya sekondari nduli ailiamua
kuomba eneo kwa ajili ya ujenzi kwa
kushirikiana na wananchi baada ya kupewa akaanza kutafuta wafadhili ambao ni
wadau wa elimu ndipo kanisa la Orthodox lilikubali kubeba majukumu kujitolea
kujenga.
“”Ninapenda kuushukuru uongozi wa kanisa la
Orthodox kupitia Askofu Tanzania kwa kukubali
kufadhiri ujenzi wa madarasa na maabara ya shule ya sekondari na kutoa msaada
wa chakula na vifaa vya shule katika kata yangu’’.alisema
Alisema kutokana na
kukithiri kwa kwa vitendo vya
ubakwaji kwa watoto wa kike na kupata mimba za utotoni kwasababu ya umbali, shule hiyo itasaidia
kutatua changamoto hiyo iliyokuwa inawasumbua kwa muda mrefu.
Diwani huyo aliishukuru
serikali ya mkoa na wilaya kwa kushirikiana pamoja kutafuta eneo kwa ajili ya zoezi hilo na hatimae wakafanikiwa kupata eneo lenye kilomita 17 ambalo lilitolewa na Shafii Haji mkazi wa
mkoa wa Iringa.
Naye askofu mkuu wa kanisa la Orthodox[Irinoupolis Tanzania
Dimitrios Zachalegas amewataka wadau wa maendeleo
nchini wametakiwa kujitoa katika
shuguli za maendeleo kwa kuwekeza katika
sekta mbalimbali ili kuleta chachu katika maendeleo nchini.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha mgongo
kata ya Nduli wilaya ya Iringa katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa shule ya sekondari inayojengwa chini ya ufadhiri wa kanisa hilo .
Dimitrios alisema kutokana
na kuona umuhimu wa Elimu kwa watoto
nchini kanisa hilo limejitolea kuunga juhudi za serikali kujenga shule ya
sekondari katika eneo la Mtagala katikakati ya kijiji cha Mgongo ili wananchi wanaozunguka waweze kunufaika na wanafunzi
waweze kupata Elimu kwa uraisi zaidi.
Alisema shule hiyo inatakiwa
kujengwa muda wa miezi sita tu pamoja na maabara kuanzia sasa ili kuendana na
kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Dr. John.Pombe Magufuli
kuhusu utekelezaji wa Elimu ya msingi na sekondari bila malipo.
Askofu alisema kuwa kwa mkoa
wa Iringa kanisa hilo limeweza kujenga shule 4 za sekondari ikiwemo hiyo
inayotarajiwa kujengwa katika kata ya nduli kijiji cha Mgongo
‘’Tumejenga shule ya
sekondari Ilolasimba,Kidamali,St.Marcus,Dimitris pamoja hii tunayotarajia kuanza ujenzi hivi
punde na tutaendelea kuisaidia serikali kutoa huduma tofauti katika jamii
kulingana na mahitaji ya eneo husika’’ Alisema
Pamoja na uwekaji wa jiwe la
msingi la ujenzi wa shule ya sekondari viongozi hao waligawa msaada wa chakula
tone tatu,sawa na gunia 30 yenye tamani
ya 1754500 kwa wananchi wa kijiji cha na kusema kuwa serikali haiwezi kujitoa kwa kila kitu
kuwakilimia wananchi bali mashirika na asasai zisizo za serikali zinapaswa
kutoa michango yao katia jamii na kuachana na dhana ya kuiachia serikali pekee.
Aidha alitoa msaada wa
daftari kwa wanafunzi,begi za kubebea daftari ,viatu aina ya yeboyebo kwa kila
motto,biscuit .pipi pamoja na kutoa huduma ya afya kwa kuwatibu wagonjwa ambao
walifika kupokea msaada wa chakula na wakapata matibabu.
Akitoa neno la shukrani kwa
uongozi wa kanisa hilo Diwani wa kata ya Nduli
Basher mtove alisema
ninawashukuru wafadhiri kutoka kanisa la
Orthodox kwa kujitolea kujenga shule ya sekondari pamoja na maabara,na kuwataka waendelee
kuisaidia serikali bila kuchoka.
Alisema baada ya kuona adha kubwa kutembea kwa umbali
zaidi ya kilomitre 7 kwenda kupata elimu ya sekondari nduli ailiamua kuomba
eneo kwa ajili ya ujenzi kwa
kushirikiana na wananchi baada ya kupewa akaanza kutafuta wafadhili ambao ni wadau
wa elimu ndipo kanisa la Orthodox lilikubali kubeba majukumu kujitolea kujenga.
“”Ninapenda kuushukuru uongozi wa kanisa la
Orthodox kupitia Askofu Tanzania kwa kukubali
kufadhiri ujenzi wa madarasa na maabara ya shule ya sekondari na kutoa msaada
wa chakula na vifaa vya shule katika kata yangu’’.alisema
Alisema kutokana na
kukithiri kwa kwa vitendo vya
ubakwaji kwa watoto wa kike na kupata mimba za utotoni kwasababu ya umbali, shule hiyo itasaidia
kutatua changamoto hiyo iliyokuwa inawasumbua kwa muda mrefu.
Diwani huyo aliishukuru serikali
ya mkoa na wilaya kwa kushirikiana pamoja kutafuta eneo kwa ajili ya zoezi hilo na hatimae wakafanikiwa kupata eneo lenye kilomita 17 ambalo lilitolewa na Shafii Haji mkazi wa
mkoa wa Iringa.
0 comments:
Post a Comment