Watu
tisa wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kutungua helikopta iliyokuwa
ikifanya doria kwenye Pori la Akiba la Maswa wilayani Meatu, Simiyu na
na kumuua rubani wake.
Mbali na kutungua chopa na kumuua rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza, watu hao pia wameshtakiwa kwa kukutwa na nyara za Serikali, kuuza na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Washtakiwa
hao walifikishwa mbele ya Mahakama ya Mkoa wa Simiyu jana wakiwa chini
ya ulinzi mkali wa polisi, huku umati wa wananchi wakifurika na
kusababisha hekaheka mahakamani hapo.
Yamiko
Mlekano, ambaye ni wakili mwandamizi wa Serikali, alidai kuwa
washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi tatu; uhujumu uchumi,
mauaji na umiliki wa silaha bila ya kibali.
Katika
kesi namba mbili ya mauaji, Wakili Yamiko alidai kuwa Shija Mjika (38),
Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42) na Moses Mandagu walitungua
helikopta hiyo Januari 29 kwenye Hifadhi ya Mwiba iliyoko Kijiji cha
Makao wilayani Meatu na kumuua rubani Gower.
Mlekano
alidai kuwa katika kesi ya uhujumu, mshtakiwa namba moja Iddy Mashaka
(49) anadaiwa kujihusisha na kuratibu tukio la uhujumu uchumi kinyume na
sheria.
Mbele
ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, John Nkwabi, wakili huyo alida
kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 6 na Februari Mosi wilayani
Meatu kwa kumshauri mshtakiwa namba mbili, Shija Mjika (38) kuua wanyama
wasioruhusiwa.
Katika
shtaka la pili, watu saba; Njile Gunga (28), Dotto Pangali (42), Moses
Mandagu (48), Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40), Mapolu Njige (50) na
Mange Barumu (47) pia wanashtakiwa kwa kuhujumu uchumi.
Aliieleza
mahakama kuwa kati ya Januari 21 na 29 katika wilayani Meatu,
washtakiwa walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo
bila ya kibali cha Serikali.
Wakili
Mlekano alidai kuwa shtaka la tatu la uwindaji wanyama wasioruhusiwa
linawakabili mshtakiwa wa pili hadi tisa na wanadaiwa kutenda Januari 26
na 29 kwenye Hifadhi ya Mwiba Kijiji cha Makao wilayani Meatu wa kumuua
tembo mwenye thamani ya Sh32,891,100 bila ya kibali.
Katika shtaka la nne, mshtakiwa namba mbili na tisa wanatuhumiwa kumiliki nyara za Serikali kinyume na sheria.
Washtakiwa
wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari 29 na Februari Mosi wilayani Meatu
ambako walikamatwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo 31 na thamani ya
Sh32,891,100.
Katika
shtaka namba tano, Mashaka na Mjika wanashtakiwa kwa kuuzaji nyara za
Serikali kinyume na sheria na kwamba walitenda kosa hilo kati ya Januari
6 na Februari Mosi wilayani Meatu.
Hakimu
Nkwabi alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na
mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na aliahirisha
hadi Februari 24 zitakapotajwa tena.
Katika
kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na silaha kinyume cha sheria iliyosomwa
mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya, Mary Mrio, washtakiwa wanakabiliwa
na mashtaka matano.
Washtakiwa
hao ni Buluma, Mjika, Pangani, Ngunga, Mandagu, Huya na Kanga ambao
baadhi yao walikiri kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria akiwamo
Njile anayedaiwa kutungua helikopta hiyo.
Washtakiwa
hao walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na bunduki aina ya
Riffle 303, wakati Ngunga na Mandagu walikiri shtaka la tatu, nne na
tano la kukutwa na silaha na risasi bila ya kibali.
Hata
hivyo, Hakimu Mrio alishindwa kutoa hukumu kwa washtakiwa waliokiri
kosa kutokana na kutokuwapo kwa vielelezo mahakamani hapo, hivyo kesi
hiyo iliahirishwa hadi leo.
Watuhumiwa
wakiwa ndani ya gari la polisi, baada ya kufikishwa kituo cha polisi
Bariadi wakitokea wilayani Meatu kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Njile Gunga
(28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la Akiba
la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika tukio
hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku
Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
Iddy
Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha Interejensia
katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa kiunganishi
Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi leo hii.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo akionyeshwa watuhumiwa wa ujangili ambao walihusika kutungua Helkopta.
Watuhumiwa wakiwa Mahakamani.
Wakazi wa Mji wa Bariadi wakiwa wamefurika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya hiyo kushuhudia watuhumiwa hao.
0 comments:
Post a Comment