Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga |
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kesi ya
kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wake ubunge jimbo la Iringa
Mjini, Frederick Mwakalebela iko pale pale, kikipinga taarifa zilizosambazwa
kwenye mitandao ya kijamii jana na kuchapwa katika baadhi ya magazeti leo
kwamba kesi hiyo imefutwa.
Akizungumza na wanahabari hii leo, Katibu
wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema; “kwa mambo yanayohusu sheria ni
kawaida sana hata kwa wanasheria wenyewe kufanya makosa ya kiufundi.”
Mtenga alisema katika shauri lao la awali
ambalo wanalifanyia marekebisho hawakumuingiza mwanasheria mkuu wa serikali
katika orodha ya wanaoshitakiwa.
“Tumewaiteni wanahabari tuwaambieni
kwamba Msigwa hajashinda kesi. Kesi ipo na tungependa wananchi wajue kwamba
kesi ya msingi ipo na inaendelea,” alisema.
Alisema; “Msigwa hawezi kushinda kesi
kwenye FaceBook, wala kwenye magazeti, kwa mujibu wa sheria atashinda kesi hizo
pale tu ambapo mahakama itatimiza wajibu wake kwa kutoa haki.”
Naye Mwakalebela alisema shauri lake la
kupinga ushindi wa Mchungaji Msigwa limekuwa likipata mapingamizi mengi.
“Pingamizi lingine ni baada ya
mwanasheria wangu kutomuweka mwanasheria mkuu wa serikali na hivyo maahakam
kuliondoa ili likarekebishwe,” alisema.
Kuondolewa kwa shauri hilo mahakamani
haina maana kwamba limefutwa kama ilivyotasfiriwa na upande wa pilia na ndio
maana mahakama hiyo hiyo imewapa fursa ya kulirudisha tena mahakamani.
“Kwa sasa wanasheria wetu wanalifanyia
kazi hilo vizuri ili litakaporudi mahakamani kusiwepo na dosari zingine na
badala yake lianze kusikilizwa,” alisema.
Alisema kesi hiyo ya kupinga matokeo
itamalizwa kwa pande zote kusikilizwa ili haki itendeke na sio kwa maamuzi ya
propaganda.
0 comments:
Post a Comment