Mkurugenzi mkuu wa Green Resources ambao ni kampuni tanzu
ya sao hill industry akifafanua jambo kwa cosato chumi mbunge wa mafinga mjini
wa pili kulia, Denis kutemile anayefuatia na Hezron Vuhahula ambaye ni katibu
wa mbunge
Aloyce mbisha meneja mipango akimuelekeza jambo cosato
chumi wapili kushoto Wakati wa ziara ya kikazi kwenye kiwanda cha sao hill
mafinga. Kulia ni Denis kutemile diwani wa kata ya sao hill na kushoto ni
Hezron Vuhahula katibu wa mbunge
Vijana katika kiwanda
cha sao hill wakipanga mbao baada kutoka kwenye mashine ya kichabi
baadhi ya nguzo
zikiwatayari kusafirishwa maeneo tofauti tofaiti
Mbunge
wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amefanya ziara katika Taasisi za Umma na
Binafsi, kama Sao Hill Industries, Sao Hill Forest, Kiwanda cha Pareto na
kampuni ya simu ya TTCL, Polisi, PCCB, NSSF na Bank za Mucoba, NMB,CEDB, magereza
na atamalizia katika taasisi za elimu.
Akizungumza
na blog hii Chumi alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha katika
maeneo hayo pamoja na kujua changamoto gani wanazokumbana nazo wakati wa
utendaji kazi wao.
“Nataka
mafinga iwe ya kipekee kwa kuitengenezea mikakati maalumu ya kuleta maendleo ya
haraka na kuwa mipango endelevu yenye faida kwa wananchi wangu unajua hili
jimbo ni jimpya hivyo linachangamoto nyingi”.alisema chumi
Aidha
Chumi ametembelea baadhi ya viwanda ambavyo vipo katika jimbo la mafinga na
kujionea changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watendaji wa viwanda hivyo
pamoja changamoto za uendeshaji wa viwanda hivyo.
“Nilipo
fika katika kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini ya Kampuni ya Pyrethrum
Company of Tanzania (PCT) nimekutana na changamoto kubwa ya umeme ambayo
inawakwamisha katika zoezi zima la uzalishaji mali kutoka kiwanda hicho cha
pareto”.alisema chumi
Chumi
ameendelea kusema kuwa tatizo la umeme limeonekana kuwa kubwa kutokana na
viwanda vyote alivyotembea kumlalamikia tatizo hilo na kumuomba awasaidie
kulitafutia ufumbuzi ili kuongeza uzalishaji wa mali na kuongeza pato la mji wa mafinga.
“Nitalifaatilia na kujua nini tatizo ili
tuweze kulitatua na kuwafanya mzalishe kwa wingi na muongeze ajira kwa wananchi
wazao”.alisema chumi
Naye
Kaimu Meneja Mkuu William Kufakwepasi wa kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini
ya Kampuni ya Pyrethrum Company of Tanzania (PCT) amesema kuwa wamekuwa
wakiwalipa mishahara wafanyakazi bila kufanya kazi kutokana na tatizo la umeme
hivyo wamekuwa wakipata hasara kubwa,na kumuomba mbunge wa jimbo hilo la
mafinga mjini cosato chumi kuwasaidia kutatua tatizo hilo.
Hata
hivyo Bi Roselyne Mariki wa Green Resources (sao Hill Industries), wanaomba
kuwepo Sub Station ya Umeme kwa sababu wanachukulia Umeme unaotoka Mgololo na ule
wa kutoka Mafinga umekuwa unapungua sana nguvu na kupoteza asilimia 30% ya muda
wa kufanya kazi kutokana na kukatika kwa umeme lakini wafanyakazi wanaendelea
kulipwa.
0 comments:
Post a Comment