Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
limepitisha bajeti ya zaidi ya Sh. 67,613,232,516 Katika
kikao maalum cha baraza la Madiwani kwa mwaka 2016/2017
ikiwa ni makisio ya mwaka mpya wa fedha utakaoanza mwezi wa 07 mwaka huu.
Makisio ya bajeti hiyo
yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambazo makusanyo ya ndani yanayokadiliwa
kufikia kiasi cha jumla Sh.4,189,145,436
, ruzuku kutoka serikali kuu zaidi ya 44,063,827,880 ambazo ni kwa ajili ya
mishahara na matumizi ya kawaida, huku miradi ya maendeleo ikiwa na jumla ya sh.21,294,808,400
Akiizungumzia bajeti hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
Wilaya ya Mufindi Bi. SAADA MALUNDE, amebainisha kuwa, Halmashauri imeanzisha
vyanzo vipya vya mapato amabapo kuanzia mwaka wa Fedha 2016/2017 Halmashauri
inataraji kuanza kutoza kodi za majengo kwa wakazi wake pamoja na tozo ya
ushauru wa madini kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa kwa lengo la kuongeza
mapato ya ndani.
“Huwezi kutoza kodi au
ushuru wowote pasipo kutoa elimu kwa jamii, baada ya baraza kuridhia, sisi kama
watendaji tunajipanga kwenda kutoa welimu kwa umma ambapo, tutaenda kwenye kila
kata na kutoa elimu kweye kamati za maendeleo za kata kisha halmashauri za
vijiji na hatimaye kwenye mikutano mikuu ya vijiji ili wananchi waweze kufahamu
kabla ya kuanza kutoza mapema mwezi wa saba”
Kizungumza wakati akifunga kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wiaya Mufindi FESTO MGINA, metoa rai kwa Madiwani
na wataalam wa Halmashauri ya Mufindi kuhakikisha kwa pamoja, wanashirikiana
katika suala la ukusanyaji wa mapato mara baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa Fedha
ili Halmashauri iweze kufikia malengo na kutoa huduma kwa jamii.
Aidha, Mgina ametanabaisha kuwa, pamoja na randama ya bajeti
hiyo kwa mwaka ujao wa Fedha, Halmashauri imeambatisha maombi maalum kwa
sirikali kuu ambayo ni pamoja ombi la shilingi Sh. 550,000,000 kwa ajili ya
ukarati wa shule ya Malangali ikiwa ni
miongoni mwa shule kongwe hapa nchini ambazo viongozi wengi wa Taifa hili
walipata kusoma Sanjari na ombi la
kupatiwa magari matatu yenye thamani ya Sh.540,000,000 maalum kwa ajili
kusafirishia wagonjwa ambayo yatasambazwa katika vituo vitatu vya afya vilivyopo
tarafa za Sadani, Ifwagi na Kasanga.
0 comments:
Post a Comment