Thursday, February 4, 2016

WAZAZI WATAKIWA KUWAPELEKA WATOTO WENYE ULEMAVU SHULENI


Wazazi na walezi wametakiwa kuachana na kasumba ya kuwaficha majumbani watoto wenye  ulemavu na badala yake  kuwapeleka shule   kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadaye hasa hasa katika kipindi hichi ambacho elimu ni bure.
Kauli hiyo imetolewa na katibu wa uwt wilaya ya kilolo Judith Laizer wakati jumuiya hiyo ilipokwenda kutoa msaada katika  familia moja yenye  watoto wenyeulemavu watatu wakati wa  kushererekea miaka 39 ya chama cha mapinduzi  Ccm
Laizer alisema kuwa ni vema wazazi wakawafichua watoto waliofichwa majumbani na kuwapeleka shule kwa ajili ya kupata elimu kwani kumekuwepo tabia ya  wazazi na walezi wanaowaficha watoto wa kwa kuwa ni walemavu kwa kuona aibu kuwa jamii itawatenga  

Alisema mtoto ni Baraka kutoka kwa mungu na hauwezi kumpangia mungu akulete mtoto wa namna gani hivyo endapo kuna mazizi anamtoto mlemavu hapaswi kujiona mwenye mkosi bali anapaswa kumtunza na kumlea kwani naye ni binadamu kama walivyo binadamu

“Nimeitembelea familia hii nimeumia sana kwani maisha wanayoishi ni ya shida sana hawana msaada wowote nyumba yao inavuja hawana chakula  maisha yao ni ya kuunganga unga mpka watu  waje kama sisi kuwaletea vitu  vidogo vidogo kama mchele na mafuta na mbaya Zaidi hata watoto hao wote watatu hakuna hata mmoja aliyewahi kukanyaga shule ingawa wanaonekana ni wakubwa hivyo jamii tu napaswa kuwasaidia watoto hawa”

Alisema jumuiya hiyo pamoja na wadau mbalimbali watahakikisha  kusaidia na kwa pamoja ili kuweza kuwasaidia watoto hao kuweza kuwa na mahali kwa kukaa kwa kuwa wanaishi maisha ya shida kwa kukaa katika nyumba ya matope iliyoezekwa kwa nyasi .

Akishukuru kwa shida kwa kuwa sauti yake haitoki vizuri baada ya kupokea msada wa vitu mbalimbali vya kula Jenifa mpogole aliwashukuru akinamama hao huku akiwaomba wamsaidi ili aweze kwenda shule kwa kuwa anahitaji kuja kuwa fundi cherehani.

Kwa upande wake mwenyekiti wa  kitongoji cha ilala C Kihongozi alisema kuwa kwa  kushirikiana na wanakitongoji wenzake wake mbioni kufetua matofali ili kuweza kujenga nyumba itakayowasaidia kukaa mana kuna  muhisani aliamua kujitolea bati za kuezekea nyumba hiyo

Mbali na kutembelea familia hiyo pia jumuiya hiyo ili kwenda kufanya usafi katika hospiyali ya wilaya ya kilolo  pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa zikiwemo sabuni mafuta mapoja na dawa za kufanyia usafi .
Picha no tud 1 png (1,654k)ni katibu wa jumuiya ya UWT wilaya ya kilolo Judith Lasizey wa pili kutoka kulia akiwana wa nawake wenzake wa jumiya hiyo walipotembelea familia yenye watoto watatu walemavu ikiwa ni maadhimisho ya miaka 39 ya chama cha mapinduzi hivi karibuni

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More