JENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma jana limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa
Akizungumzia
kutekeleza kwa jengo hilo Meneja wa Posta Mkoa wa Dodoma, Magreth
Mlyomi alisema mpaka sasa kuna hasara kubwa kutokana na kutekeleza jengo
hilo sambamba na vifaa vyote vya ofisi.
Mlyomi
alisema licha ya kuwa hakuna mfanyakazi hata mmoja aliyepoteza maisha
katika jengo hilo lakini mpaka sasa kuna vitendea kazi vingi vya ofisi
pamoja na mizigo ya wateja imeteketea.
“Kuna
mizigo mingi pamoja na vifaa vya kazi vyote vimeteketezwa na moto na
kwa taarifa nilizopata kulikuwa na mizigo ya watu, inaonesha kuwa chanzo
cha moto ni umeme,” alieleza Meneja huyo.
Akizungumzia
kuhusu masuala ya miundombinu ya maeneo husika alisema ni mibovu na
kutokana na changamoto hiyo suala hilo lipo katika mamlaka husika ya
manispaa.
Kwa
upande wake katibu wa wafanyabiashara katika soko la Sabasaba katika
Manispaa ya Dodoma, Gergod Lugusi alisema jana saa nne asubuhi kulitokea
moto mkali ambao uliunguza jengo hilo.
Alisema
chanzo cha moto huo inasemakana kuwa ni tatizo la umeme na uongozi
ulilazimika kutoa taarifa katika kikosi cha zima moto na bila kuchelewa
walifika kwa wakati.
Hata
hivyo alisema licha ya kufika kwa wakati katika tukio bado kikosi hicho
kilikutana na kikwazo kwa kutokana na miundombinu kuwa mibovu na migumu
kupitika.
0 comments:
Post a Comment