Monday, February 8, 2016

CHUO KIKUU CHA AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA PILI NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu Mkuu wa Chuo cha African Graduate University, Askofu Profesa Stephano Nzowa (kulia), akizungumza katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia na mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo, ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia katika mahafali hayo.
 Wahitimu wa chuo hicho wakiwa wamejipanga tayari kwa kuingia ndani kuanza kwa shughuli mbalimbali za mahafali hayo.
 Ndugu na jamaa na wageni waalikwa  kwenye mahafali hayo.

 Wahitimu hao wakishiriki kuimba wimbo wa taifa.
 Mahafali yakiendelea.
 Taswira katika ukumbi wa mahafali.
 Waliotoa huduma katika mahafali hayo wakiwa katika pozi.
 Waimbaji wa nyimbo za injili wakitoa burudani.
 Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo akimpongeza mwimbaji Stella Joel kwa kupata tuzo hiyo.



Na Dotto Mwaibale

WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha African Graduate University katika ngazi mbalimbali wametakiwa kutumia elimu waliyopata kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringomgeni aliye kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.

"Nawaombeni sana elimu mliyopata itumieni kwa ajili ya kuinua maisha ya familia zetu, wananchi na taifa kwa ujumla na si vinginevyo" alisema Dk.Ringo.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Askofu Profesa Stephano Nzowa aliwata wahitimu hao kuendelea kujiendeleza kielimu hadi kufikia ngazi mbalimbali za juu.

Nzowa alisema watu wengi wamekuwa wakijiendeleza kielimu wakiwa na matumaini ya kuja kupata kazi nzuri jambo ambalo alisema ni bahati.

"Msisome kwa ajili ya kuja kupata kazi nzuri bali someni ili kujiongezea uelewa wa mambo mengi ambayo yatawasaidieni kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia fedha" alisema Nzowa.

Profesa Nzowa alisema chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sieralaoni kipo katika nchi kadhaa barani Afrika na kwa Tanzania kinajengwa Wanging'ombe mkoani Njombe na kuwa mahafali hayo ni ya 25 na kwa hapa nchini ni ya pili.


Mkuu wa chuo hicho Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia alisema lengo lao ni kufungua chuo hicho katika nchi mbalimbali duniani ili wanafunzi kujua mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii na ya mungu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More