Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amesema kuwa chama
chake kitawachambua na kuwaadhibu wote ambao walikisaliti katika
Uchaguzi Mkuu uliopita, kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa hadi
Taifa.
Dk.
Kikwete ametoa kauli hiyo Jumatatu ya wiki hii mjini Kibaha
alipohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi mpya ya chama hicho mjini
humo.
“Baada
ya mchakato wa Dodoma wapo ambao walisusa kabisa na wakawa wanajificha.
Unakuta hahudhurii mikutano yetu ya kampeni, lakini ya wenzetu upinzani
unamkuta na akiulizwa anasema eti alialikwa,” alisema na kusisitiza kuwa wanachama kama hao ni wasaliti na uanachama wao una mashaka.
Kikwete
alisema mchakato wa kuwaadhibu wanachama wasaliti utafanyika wakati
wowote baada ya kuyapitia majina ya wote wanaotuhumiwa kukihujumu chama.
“Tayari
tuna majina ya watu ambayo yanadhaniwa walikihujumu chama. Tutayapembua
katika vikao mbalimbali halali kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya,
mkoa na Taifa na tutaamua kwa haki wakati wa kuwaadhibu,” alisema.
Aliwataka
wanachama hao kufanya tathmini na kutambua waliokisaliti chama lakini
alionya vikao vya kuwabaini vitende haki bila kumuonea mtu akisema yapo
baadhi ya majina yanatajwa kuwa ni wasaliti kutokana na migogoro binafsi
baina yao.
0 comments:
Post a Comment