Monday, February 8, 2016

WAKAZI wa Wilaya ya Mafinga Mkoani Iringa wametakiwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF)

WAKAZI wa Wilaya ya Mafinga  Mkoani Iringa  wametakiwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili waweze kupatiwa matibabu kwa kuchangia sh10,000 na kupatiwa dazi maalumu itakayowawezesha kupata matibabu mwaka mzima kwa kaya yenye watu sita.


Akizungumza kwenye kijiji Sadani watati wa sherehe za kutimiza mika 39 ya chama cha mapinduzi CCM  mkuu wa wilaya hiyo Jowika Kasunga alisema kuwa ni vema kaya nyingi kujiunga na mfuko huo ili kuepuka adha ya kupata matibabu pindi unapopata mgonjwa katika kaya .


alisema tatizo la ukosefu wa dawa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitalini litamalizika, endapo kaya nyingi zikijiunga na CHF kwani serikali nayo itaweka mkono wake ili kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa.


Alisema kuwa huduma hiyo ya CHF itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa watu waishio vijijini kwani wakati mwingine kaya nyingine hushidwa kulipia garama za matibabu kwa kuwa ni kubwa lakini endapo watajiunga na mfuko
huo itakuwa ni mkombozi katika maisha yao.

alisema kila kaya wilayani humo inapaswa kuchangia sh10,000 za gharama za matibabu ili watibiwe kwa kadi na kuachana na mtindo wa kutibiwa kwa fedha.

“Leo tumekuja hapa kusheherekea sherehe za CCM lakini tukipata nafasi inabidi tusema tuu mana ni wakati wa kuchapa kazi hivyo ndugu zangu Kaya moja ikilipa sh10,00 inapatiwa matibabu kwa mwaka na isipougua inakuwa imewachangia wenzao watakaougua, kwani hata kwenye bima za magari na pikipiki wasiopata ajali wanawachangia waliopata majanga,” alisema Kasunga .

Kasunga  alisema mwanachama wa CHF watanufaika na huduma zote za afya za msingi na kinga na tiba kwa zahanati, kituo cha afya na hospitali bila ya kuangalia ugonjwa anauomwa au mgonjwa ama garama zake ‘ Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama alisema
watanzania wamepata neema kutoka kwa mungu kwa kuwapatia kiongozi shupavu kama Raisi John Mgufuli kwani kiongozi huyo amakuja kuwakomboa watanzania waliokuwa wamepoteza matumiani katika nchi yao .


Mgahama alisema kuwa huu ni wakati wa kuchapa kazi bila ya kuangalia itikazidi za  vyama kwani wakati wa kampeni ulikwisha pita na wananchi wakachagua viongozi kutoka katika chama hicho na sasa kilichobaki ni kutekeleza yale waliyowaahidi watanzania “Ndugu zangu leo chama kinatimiza miaka 39 tangu kuzaliwa tumebahatika kupata kiongozi bora kama magufuli tunapaswa kutembea kifua mbele kwa kuwa anatekeleza yale wananchi waliokuwa wanataka mi naombeni tumuombe Risi wetu kwani kazi ya kutumbua majipu siyo kazi ndogo bali ni vita kubwa kuliko vita yoyote ileee unayoidhania ‘’.


Alisema kuwa kwa  sasa Tanzania imegeuka kuwa nchi ya mfano kwani baadhi ya nchi hutuma watu wao kuja kujifunza uongozi uliotukuka wa Raisi Magufuli anavyoongoza nchi  hivyo ni jambo la kuigwa na la mfano.


Hata hivyo Muhagama aliwataka wazazi na walezi kumuunga mkono Raisi Magufuli kwa kupeleka watoto wao shule kwa kuwa elimu ni bure ili waweze kupata elimu itakayokuja kuwasaidia katika maisha yao ya hapo badaye .


Kwa upande wake mwenyekiti wa halimashauri ya mji wa Mafinga Festo Mgina aliwakumbusha wananchi kuweza kuwajibika katika kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato ikiwemo kilomo ili kujikwamua katika
wimbi la umaskni.


Alisema kuwa ili dhana ya Raisi Magufuli ya HAPA KAZI TU iweze kutimia ni vema kila mtu kuwajibika katika nafasi yake aliyopo ili malengo ya kupunguza umaskini na kuongeza kipato iweze kutimia “Mkulima nenda shambani ,mfanyabiashara nenda huko na watumishi wa serekali wajibikeni katika nafasi zenu hakika hii nchi itakuwa ni ya asali na maziwa alisema”” Mginaa


Katika sherehe hizo chama cha mapinduzi wikayani humo kwa kushirikiana na wanachi walishiriki zoezi la ufanyaji usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye zahanati na mashuleni

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More