Monday, February 29, 2016

Kikwete: Nitaachia Uenyekiti wa CCM, Lakini Sitaacha Vikao vya Ndani CCM

Moja kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha operesheni hiyo ndani ya chama hicho.

Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete amesema kuwa ataachia nafasi hiyo hivi karibuni na kumkabidhi Rais Magufuli, lakini alitoa angalizo kuhusu uhusika wake kwenye chama hicho baada ya kujivua kofia hiyo nzito.

Ingawa Katiba ya Chama hicho inaeleza kuwa mwenyekiti mpya atapatikana mwaka 2017, Mwenyekiti wa Chamo hicho, Dk. Jakaya Kikwete amepanga kuachia nafasi hiyo mapema (mwaka huu) kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.

Akiongea jana kwenye uzinduzi wa Kitabu cha maisha ya kada maarufu wa chama hicho, Marehemu Captain John Komba, Dk. Kikwete alieleza kuwa ataachia nafasi hiyo lakini hataacha kushiriki vikao vya ndani na mambo ya maamuzi ya chama hicho.

“Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nitaachia, lakini mambo ya ndani yanayohusu chama hiki sitaacha kushiriki,” alisema.

Februari mwaka huu, Dk. Kikwete aliwaambia wazee wa CCM mjini Singida kuwa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa chama hicho mwaka huu, zilikuwa sherehe zake za mwisho akiwa kama Mwenyekiti.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More