Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) imeunda kanuni zitakazowaongoza
wabunge wake kuendesha shughuli mbalimbali za chombo hicho cha
uwakilishi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu
aliwaambia wanahabari jana kuwa kanuni hizo ambazo zimeundwa kwa
kushirikisha vyama vyote vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa)
zitasaidia kuondoa holela iliyokuwa ikijitokeza awali ndani ya KUB.
Mwalimu,
ambaye chama chake ndiyo kinaongoza kambi hiyo, alisema Chadema
inaipongeza hatua hiyo kwa kuwa imeonyesha kuzaa matunda katika mkutano
wa pili wa Bunge la 11 uliomalizika wiki iliyopita.
Kanuni hizo
za kambi rasmi ya upinzani, kwa mujibu wa Mwalimu zimeanzishwa kwa
kufuata kanuni ya 16, ibara ya 4 ya Kanuni za Kudumu za Bunge ambayo
inasema:
“Vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni vinaweza
kutunga kanuni za vyama vya kwa ajili ya uendeshaji bora wa shughuli za
vyama hivyo bungeni.”
Mwalimu alisema kanuni hizo tayari zimeshasaidia uteuzi wa wawakilishi katika vyombo vya kimataifa kupitia Bunge.
Alisema
katika utaratibu wa kanuni hizo mpya jambo likishaamriwa kwenye vikao
vya umoja huo hakuna mtu wa kupinga na ikitokea mbunge husika akazivunja
hatua za kinidhamu zitachukuliwa.
“Kwa sasa hamna tena songombingo ya
kupata nafasi za uwakilishi ndani ya Bunge. Likipita jambo ndani ya
caucus (kikao cha chama) basi limepita...hakuna tena kuvujisha siri
ndiyo maana safari hii hata waandishi ilikuwa vigumu kupata taarifa za
ndani,” alisema.
Akizungumzia umeya Dar es Salaam alisema kuna hila za
wazi za kutaka kuongeza wajumbe wasiotakiwa katika uchaguzi hasa kutoka
Ilala na Kinondoni.
0 comments:
Post a Comment