Tuesday, February 23, 2016

WAKULIMA WILAYANI RORYA MKOANI MARA WAPATIWA MAFUNZO YA KUPATA HUDUMA ZA UGANI KWA NJIA YA SIMU

Mtafiti Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney.

Maofisa Ugani wa Wilaya ya Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Rorya, Dominick Ndentabura akizungumza na wakulima hao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Wakulima wa Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mkulima Saye Okelo akizungumzia changamoto ya ukosefu wa mbegu katika mafunzo hayo.
Mkulima Sinde Mjinja akielezea changamoto ya bei kubwa ya pembejeo za kilimo.
Mkulima akizungumizia magonjwa ya mbegu za mhogo na pembejeo kuchelewa kuwafikia wakulima.
Mkulima Emmanuel Lugombo akizungumzia kuoza kwa mbegu ya mkombozi.
Mkulima Sophia Charles kutoka Kijiji cha Roche akizungumzia changamoto ya ukosefu wa soko la zao la mhogo ambapo wanategemea zaidi soko nchini Kenya.
Mkulima Charles Ruola akizungumzia changamoto ya kilimo cha mahindi.
Mkulima wa Kijiji cha Kowaki kilichopo Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Elias Kaseno akizungumzia changamoto ya kilimo cha muhogo na mahindi mbele ya watafiti kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliopo wilayani humo jana kujua changamoto mbalimbali za wakulima na kutoa mafunzo ya matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi akielekeza jinsi ya kupiga simu wakati akiendesha mafunzo hayo kwa wakulima.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo.
Wakulima wakiwa mafunzo hayo.
Wakulima wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wakulima hao wakibadilishana mawazo baada ya kupiga picha.
Jengo la Halmshauri ya Wilaya ya Rorya.
Shamba la muhogo lililoshambuliwa na ugonjwa wa batobato  lililopo jirani na jengo la Halmshauri ya Rorya ambapo wapo wataalamu wa kilimo.

Na Dotto Mwaibale

KATIKA hali isiyotegemewa shamba lenye ukubwa wa ekari moja la zao la muhogo lililopo nyuma ya Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambapo ofisi ya wilaya ya kilimo ipo halipo katika matunzo ya kilaalamu ambapo mwandishi wa habari hii ambaye yupo katika ziara ya kilimo na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) alitembelea. 

Mwandishi wa habari hii alidhani kuwa shamba hilo la muhogo ni maalumu kwa ajili ya kufundishia wakulima kuhusu ugonjwa unaoshambulia zao hilo ujulikanao kama batobato na athari zake kumbe ni shamba la mkulima ambalo limekosa huduma za ugani licha ya maofisa ugani kuwepo mita chache ya  eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo inapaswa wakulima wa namna hiyo kupata huduma za kilimo kutoka maeneo mengine kutokana na maofisa ugani hao kushindwa kutoa elimu ambapo shamba hilo limekuwa ni chanzo cha kueneza ugonjwa huo katika maeneo mengine.

Akizungumza katika mafunzo ya matumizi ya simu katika kilimo kwa wakulima wa wilaya ya Rorya Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi alisema mafunzo hayo ya siku moja yatawasaidia wakulima kupashana habari za kilimo na changamoto zao.

"OFAB imeleta mafunzo haya kwa wakulima ambao ni wadau wetu ili waweze kupashana habari za kilimo, changamoto zinazo wakabili na kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia ya simu badala ya kutumia simu hizo kupigiana kwa mambo ya kawaida" alisema Nyinondi.

Alisema kupitia mafunzo hayo wakulima hao wataweza kushirikiana na mitandao mingine ya kijamii ili kutatua changamoto zao za kilimo zikiwemo za wadudu waharibifu wa mazao, ukame na nyinginezo.

Alisema washiriki wa mafunzo hayo walikuwa ni 20 kutoka katika wilaya hiyo na kuwa shirikisha wataalamu wa kilimo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More