Agizo la serikali kuzuia usafiri wa bodaboda mjini umegeuka kuwa kitega uchumi kwa baadhi ya vijana walioajiriwa kuhakikisha agizo inatekelezwa.
Hii imethibitika baada ya mwandishi wa Mo Dewji Blog kufumania tukio la vijana wa jiji wakidai rushwa wazi wazi bila woga kwa mwendesha pikipiki wa magurudumu watatu maarufu kama bajaji.
Kachero wetu (jina limehifadhiwa) alifanikiwa kupata picha za wala rushwa pamoja na kunasa sauti za tukio lote.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tambaza wakiwa pembezoni ya barabara katika daraja la Salenda.
Mmoja wa mfanyakazi wa Tambaza akisimamisha bajaji.
Wafanyakazi wa Tambaza wakizungumza na dereva wa bajaji na kumuomba rushwa ya shilingi 10,000
Wafanyakazi wa Tambaza (walio na mashati ya rangi nyeupe) wakizungumza na dereva wa bajaji
Sikiliza sauti iliyorekodiwa wakati wa tukio na mwandishi wa Mo Dewji Blog
0 comments:
Post a Comment