Thursday, February 25, 2016

Mpango wa Push for Change kuwasadia Wakulima katika upatikanaji wa habari za masoko na mitaji

Kongamano la siku tatu juu ya sera ya kilimo linalotarajia kufikia tamati leo Februari 25.2016 huku likiwa limeshirikisha wadau wa kilimo Zaidi ya 150, kutoka ndani ya nje ya Tanzania wametoa maoni yao mbalimbali namna ya kuboresha kilimo hapa nchini ilikufikia maendeleo makubwa.

Kongamano hilo lililokuwa na kauli mbiu: “Mabadiliko ya sekta ya kilimo na mchango wake katika kukuza usalama wa chakula na lishe, kupunguza umasini na kuleta ajira’ limefanyika jijini Dar es Salaam ambapo wadau hao wameweza kutoa maoni yao hayo ikiwemo namna ya kufikia wakulima kwa njia teknolojia ya mawasiliano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento amebainisha kuwa masuala ya teknolojia na mawasiliano yanarahisisha upatikanaji wa habari mbalimbali ikiwemo Kilimo ambapo kampuni yake imeamua kurahisha mpango huo ilikumfikia kila Mtanzania ikiwemo hata yule wa hali ya chini kupitia mawasiliano na fursa za kupata taarifa sahihi.
Amebainisha kuwa, wakulima wanahitaji kupatiwa taarifa muhimu mbalimbali hivyo wao wameweza kuboresha huduma za teknolojia ya kufikisha habari hizo kupitia mpango wa Push for Change, ambao Mkulima kupitia simu yake hata kama ni ya kawaida anaweza kupata habari za kina juu ya masoko na namna ya kuwezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika.
Progamu ya Push For Change inatoa taarifa mbalimbali hivyo kuwa msaada mkubwa kw sekta ya kilimo. Huduma hyo pia wakulima na watu wengine wanaweza kuipata kwa kujiunga na huduma hiyo, kwa kutuma neno Change kwenda namba 15774 na kuchagua huduma unayotaka ikiwemo kupata taarifa kama Kilimo, Uchumi, biashara, afya, michezo na burudani, savei, elimu, utaliii na nyinginezo.
Aidha, kwa upande wake, Ofisa mahusiano wa wateja wadogo na wa Kati kutoka benki ya CRDB, Bi. Rehema Shambwe amebainisha kuwa wamekuwa wakitoa mikopo na ushauri kwa wakulima mbalimbali huku changamoto kubwa ni suala la mitaji kwa wengi wa wakulima hao.
Bi. Rehema Shambwe amewataka wadau na Serikali kuangalia namna ya kuweza kuboresha bidhaa zinazotoka Tanzania ilikuweza kuhimili masoko ya Kimataifa.
Imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog
Tazama video hapa:
push mobile 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento akizungumza katika mkutano huo leo Feb 25.
push jjj 
Wadau wa kilimo wakifuatilia mkutano huo ..
pushj 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Push Mobile Media Ltd, Bw. Freddie Manento akizungumza katika mkutano huo. Kulia kwake ni Profesa wa chuo cha Sheria, Arizona, Dale Beck Furnsh
push mobile3 
Ofisa mahusiano wa wateja wadogo na wa Kati kutoka benki ya CRDB, Bi. Rehema Shambwe akifafanua jambo wakati wa mkutano huo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More