Friday, July 8, 2016

WAZIRI MKUU APIGA STOP UVUNAJI MITI/MBAO KATIKA MISITU YAKE

Moja kati ya Mashamba makubwa ya mbao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza rasmi kusitisha utoaji  wa vibali vya uvunaji wa mbao kutoka katika mashamba nane ya miti ya kupandwa yanayosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Katazo hilo  limetolewa leo  (Ijumaa, Julai 8, 2016) ambapo Majaliwa  amefafanua kwamba usitishaji huo unalenga kutathmini taratibu, kanuni na vigezo sahihi vinavyotakiwa kutumika katika kugawa malighafi kutoka kwenye mashamba hayo.

Ameongeza kuwa  wadau wote wa viwanda vinavyojikita katika malighafi ya misitu na hususani wamiliki wa viwanda vya kupasua mbao wanashauriwa kuwa watulivu wakati utaratibu huu ukifanyiwa mapitio na umma utatangaziwa rasmi pindi uboreshaji huo utakapokamilika.

Aidha, Serikali  kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii inamiliki mashamba ya miti ya kupandwa 18.
Kati ya hayo uvunaji umekuwa ukifanyika katika mashamba nane ambayo ni kama ifuatavyo,

1.Sao Hill (Mufindi),
2.Buhindi (Sengerema),
3.Meru/Usa (Arumeru),
4.West Kilimanjaro (Hai),
5.Shume (Lushoto),
6.North Kilimanjaro (Rombo),
7.Kiwira (Rungwe) na
8.Kawetire (Mbeya Vijijini)

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More