Wednesday, July 27, 2016

BREAK NEWS :ASKARI POLISI ALIYEMUUA MWANAHABARI DAUDI MWANGOSI AFUNGWA JELA MIAKA 15

 

 Rais wa klub za wandishi wa habari nchini  DEOGRATIUS NSOKOLO akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kulewa kwa hukumu ya kesi ya mwanahabari daudi mwangosi



 Mke wa marehemu Daudi Mwangosi, Bi Itika akizungumza na waandishi wa habari


Mahakama kuu kanda ya iringa leo imemuhukumu kwenda jela Miaka 15 askari polisi PASIFICUS SIMONI aliyehusika na kifo cha mwanahabari wa chanel ten Daudi Mwangosi.

hukumu hiyo imetolewa leo katika mahakama mkuu kanda ya iringa

hata hivyo Mke wa marehemu Daudi Mwangosi, Bi Itika amesema kuwa anawashukuru waandishi wa habari kwa umoja waliouonesha katika kipindi chote cha kesi.

Naye Rais wa klabu za wandishi wa habari nchini  DEOGRATIUS NSOKOLO amesema kuwa amefurahishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama.

Awali wakili ambaye alikuwa anamtetea mtuhumiwa  RWEZAULA KAIJAGE amebainisha kuwa ataangalia kasoro zilizotokea wakati wa hukumu ili akate rufaa ya hukumu hiyo.

Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi wa kituo cha Channel Ten aliuawa Septemba 2, 2012 katika Kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa alipokuwa  katika majukumu ya kikazi baada ya kutokea ghasia zilizozuka kati ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na polisi katika mkutano wa chama hicho.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More