Sunday, July 10, 2016

MBUNGE VENANCE MWAMOTO AKABIDHI MABATI YENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.MOJA NA LAKI MBILI

 mbunge wa jimbo la kiloloVenance Mwamoto akikabidhi mabati 57 yenye zaidi ya Mil.moja kwa uongozi wa kata ya nyanzwa
Na fredy mgunda,Kilolo

WANANCHI wa  kata ya Nyanzwa iliyopo katika kijiji cha Nyanzwa Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa wamemuomba mbunge wa Jimbo hilo Venance Mwamoto kuwasaidia kumalizia ujenzi wa Nyumba za walimu zilizopo kwenye kata hiyo ili kuondokana na changamoto ya walimu kuishi mbali na eneo la shule.

Kilio hicho kimetolewa juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya kata hiyo ambapo wananchi hao waliamua kujitolea  nguvu kazi zao wenyewe kufyatua tofali na kuanza kujenga nyumba za walimu lakini walikwama  kumalizia ujenzi huo kutokana na kukosekana kwa rasiilimali fedha ambazo wangezitumia kununulia mabati.

Akizungumza mkazi wa kijiji hicho John Mwandi alisema kuwa pamoja na jitihada za wananchi za kufyatua tofali lengo lao ni kuhakikisha walimu wanaishi karibu za shule zao ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wanafunzi.

“Walimu wa shule nyingi za kata hii wanaishi nje ya eneo la shule hivyo kwa kuliona hilo wananchi wameamua kujitolea nguvu kazi zao kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu ili waweze kutoa huduma ili bora kwa wanafunzi.”alisema Mwandi

Naye Kauli Msisi alisema  walimu wakiishi jirani na eneo la shule litawasaidia kutoa elimu hiyo kwa ufanisi na wanafunzi wataweza kupata huduma iliyo bora na baadaye kuongeza ufaulu wao.

 “Walimu wa eneo hili walikuwa wakiishi mbali sana na shule zetu,sasa tunaona kukamilika kwa ujenzi huu walimu watakuwa hawatoki mbali,wanafunzi watapata huduma iliyobora,kiwango cha ufaulu kitaongezeka na hatimaye tutapata wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili ya kizazi cha baadaye.”alisema Msisi

Hata hivyo baada ya kuona changamoto hiyo mbunge wa jimbo hilo Venance Mwamoto alikabidhi mabati 57 yenye zaidi ya Mil.moja kwa uongozi wa kata ili waweze kumalizia ujenzi kwa haraka.

“Nimetoa mabati 40 kwa ajili ya kuezeka nyumba za walimu wa kijiji cha nyanzwa,17 kwa ajili ya kijiji cha Igunda na nimeona ni vyema nikaunga mkono kwa sababu wananchi wameshajitolea na kawaida ni kwamba serikali ndiyo inatakiwa iunge mkono kwa maana  ya halmashauri wanapofikia ngazi ya kuezeka serikali ndiyo inatakiwa kumalizia lakini mimi nimeona wanachelewa kupeleka hizo bati na hivyo kuwakatisha tama.”alisema Mwamoto

Kwa upande wake ofisa mtendaji wa kata hiyo Kimwaga Edcoss alimshukuru mbunge huyo na kuongeza kuwa mbunge alijitokeza kwenye mkutano na ndipo wananchi waliomba kusaidiwa na haikuwa ahadi yake.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More