Wednesday, July 27, 2016

RAIS MAGUFULI KUZURU MKOA WA SINGIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anayetaraji kuwasili Mkoani humo tarehe 29 mwezi huu.


Na Mathias Canal, Singida

Kutochangia maendeleo yatajwa kuwa Njia mojawapo ya kukiuka haki za binadamu, kwani wananchi wasipopata huduma bora za kijamii wanailaumu serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Jumanne Mtaturu ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anayetaraji kuwasili Mkoani humo tarehe 29 mwezi huu.

Rais Magufuli atafanya ziara ya katika Wilaya hiyo Mkoani humo ambapo kabla ya kuwasili Wilayani Ikungi atazuru Wilayani Manyoni akitokea Mkoani Dodoma.

Rais Magufuli yupo katika Chereko ya kumbukumbu nzuri ya ushindi wa Asilimia mia moja aliyoipata mwishoni mwa Juma wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na wajumbe wote wa chama hicho.


Hii ni ziara yake ya awali kuzuru Mkoani Singida tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya tano Octoba mwaka Jana na tangu awe Kiongozi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More