Sunday, July 31, 2016

MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA MJINI COSATO CHUMI AMESAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA NGO YA WORLD SHARE YA NCHINI KOREA


Afisa wa NGO ya world share ya nchini korea Nara Kim na mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi wakisaini mkataba wa makubaliano ya kazi


Afisa wa NGO ya world share ya nchini korea Nara Kim na mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi wakionyesha sehemu ya mkataba huo.
 Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young akionyesha
taa ndogo za solar kwa ajiri ya kaya masikini katika vijiji ambayo havijafikwa na umeme.
na fredy mgunda,iringa

mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amesaini mkataba wa ushirikiano na NGO ya world share ya nchini korea ,NGO hiyo inajishughurisha na utoaji wa misaada ya ujimbaji wa visima,ujenzi wa tower pamoja na mfumo wa maji katika shule za msingi.

akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo mbunge huyo amesema kuwa watashirikiana katika kuwasidia watoto yatima,watu wenye ulbino,taa ndogo za solar kwa ajiri ya kaya masikini katika vijiji ambayo havijafikwa na umeme.

Makubaliano yamefanyika jana ikiwa ni siku moja tu baada taasisi hiyo kuahidi kushughulikia tatizo la maji katika shule ya msingi ya Makalala Mchanganyiko ya mjini Mafinga.

Akitoa ahadi hiyo mbele ya Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young aliyetembelea jimbo hilo kwa mwaliko wa mbunge wake, Cosato Chumi, afisa wa taasisi hiyo Nara Kim alisema:

“Tutatoa msaada huo kama tutahakikishiwa kuondolewa vikwazo vya askari wa usalama barabarani wakati tukisafirisha mtambo wa kuchimba visima toka Dar es Salaam.
 
Alisema taasisi hiyo inayofanya kazi zake nyingi jijini Dar es Salaam inahofia kupata kadhia kutoka kwa askari hao kama inavyotokea mara kwa mara katika jiji hilo.

Akishukuru kwa ahadi ya taasisi hiyo, Mbunge Chumi aliahidi kuzungumza na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga ili kuona namna taasisi hiyo kwa kuzingatia sheria za barabarani itakavyosaidiwa ili itekeleze ahadi  hiyo.

“Nimshukuru Chumi kwasababu bila ombi lake huenda nisingefika Mafinga hii leo na kusingekuwa na makubaliano na misaada hii,” alisema Balozi wa Korea wakati akizungumza na jumuiya ya shule hiyo na kaya za kijiji cha Mtula.

Mbali na kukabidhi msaada wa mafuta maalumu ya ngozi kwa wanafunzi wenye ualbino katika shule hiyo, alikabidhi msaada wa taa 400 zinazotumia mionzi ya jua zilizotolewa shuleni, zahanati ya Mtula na kwa kaya masikini katika kijiji cha Mtula, Bumilainga na Itimboa.

Katika ziara hiyo, balozi huyo pia alitembela skimu ya umwagiliaji ya Mtula inayoendesha na chama cha Ushirika cha Mtula chenye wanachama 68 huku ikinufaisha kaya 390 za kijiji hicho cha Mtula.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More