Wednesday, February 17, 2016

NEY WA MITEGO ATAKIWA KUOMBA RADHI



Pichani ni Msani Junaisaty daimond akiwa katika pozi mbalimbali
 NA RAYMOND MINJA IRINGA

Msani anayefanya vema katika muziki wa kizazi kipya kutoka mkoani Iringa  Junaisaty Daimond (JUNAY)a memtaka mkali wa hip hop Emanuel Elibariki  Nay wa Mitego kuomba radhi kwa watu wote aliowasema vibaya katika wimbo wake wa Shika Adabu yako kwa kuwa kila mtu anatakiwa kuheshimika kwa maisha yake aliyochagua kuishi

Akizungumza na bigwa msani huyo anayetamba na wimbo wake wa changanyachanganya alisema kila mtu anamaisha yake aliyochagua kuishi ili mradi hamkeri mtu hivyo hakuna haja ya kumdisi au kumdhalilisha mwingine  kwa kuwa tu unasehemu ya kusemea .

Junay alisema kuwa licha ya msani huyo kuwa na jina kubwa katika medali ya muziki lakini yampasa kuomba msamaha kwa kuwa aliwauzi wasani hao pamoja na mashabiki wao jambo ambalo linaweza kumfanya kushuka thamani yake mbele ya jamii iliyomzunguka

“Kumekuwa na tabia ya wasanii kuwasema wenzao vibaya kupitia muziki au watangazaji kuwasema watu vibaya kwenye radio eti kisa tu anasehemu ya kusema ni vema kila mmoja lazima aheshimu uhuru na mawazo ya mtu kwani kila mtu anahaki ya kuishi jinsi anavyotaka ili mradi havunji sheria za nchi .”

Akizungumzia sula la Ney kumchana Wema Sepetu kuwa endapo mimba yake ni kick na hatimaye mimba ya Wema kutoka alisema sio jambo jema na dhahiri teem wema watamchukia msanii huyo katika maisha yake kwani itaonekana kama mchawi wake

Hata hivyo msani huyo aliwataka wasani kuwa na ushirikiano katika shida na raha kwani wasani  wengi hasa wenye majina wamekuwa wakijisahau na kushidwa kushiriki mambo mbalimbali ya kijami kama vile misiba kwani ipo siku naye atakubwa na tatizo na kutegwa kama alivyokuwa akiwatenga wenzake katika matatizo 


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More