Thursday, February 25, 2016

Donald Trump Azidi Kupeta Mchujo wa Kugombea Kiti Cha Urais Marekani

Mgombea  urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika Jimbo la Nevada nchini Marekani, na kuzidi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.

Tajiri huyo aliyewahi  kutamka  hadharani  kuwa atawafunga  jela  Rais  Mugabe  na Mseveni, sasa ameshinda mara tatu, kufuatia ushindi wake katika Jimbo la New Hampshire na Carolina Kusini.

Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.

Maofisa wa chama hicho wamesema wanachunguza  ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.

Baadhi ya wapiga kura  pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za Trump, lakini maofisa wamesema kuwa hatua hiyo siyo kinyume na sheria

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More