Monday, February 22, 2016

BAJETI YAPITISHWA MUFINDI , STORI SAHIHI TADHALI


Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limepitisha  bajeti ya zaidi ya Sh. 67,613,232,516 Katika kikao maalum cha baraza la Madiwani kwa mwaka  2016/2017  ikiwa ni makisio ya mwaka mpya  wa fedha utakaoanza mwezi wa 07 mwaka huu. 
  

 Makisio ya bajeti hiyo yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, ambazo makusanyo ya ndani yanayokadiliwa kufikia kiasi cha  jumla  Sh.4,189,145,436 , ruzuku kutoka serikali kuu zaidi ya  44,063,827,880 ambazo ni kwa ajili ya mishahara na matumizi ya kawaida, huku miradi ya maendeleo ikiwa na jumla ya sh.21,294,808,400

Akiizungumzia bajeti hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Mufindi Bi. SAADA MALUNDE, amebainisha kuwa, Halmashauri imeanzisha vyanzo vipya vya mapato amabapo kuanzia mwaka wa Fedha 2016/2017 Halmashauri inataraji kuanza kutoza kodi za majengo kwa wakazi wake pamoja na tozo ya ushauru wa madini kwa kuzingatia vigezo vitakavyowekwa kwa lengo la kuongeza mapato ya ndani.

“Huwezi kutoza kodi au ushuru wowote pasipo kutoa elimu kwa jamii, baada ya baraza kuridhia, sisi kama watendaji tunajipanga kwenda kutoa welimu kwa umma ambapo, tutaenda kwenye kila kata na kutoa elimu kweye kamati za maendeleo za kata kisha halmashauri za vijiji na hatimaye kwenye mikutano mikuu ya vijiji ili wananchi waweze kufahamu kabla ya kuanza kutoza mapema mwezi wa saba”

Kizungumza wakati akifunga kikao cha baraza hilo,  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wiaya  Mufindi FESTO MGINA, metoa rai kwa Madiwani na wataalam wa Halmashauri ya Mufindi kuhakikisha kwa pamoja, wanashirikiana katika suala la ukusanyaji wa mapato mara baada ya kuanza kwa mwaka mpya wa Fedha ili Halmashauri iweze kufikia malengo na kutoa huduma kwa jamii.

Aidha, Mgina ametanabaisha kuwa, pamoja na randama ya bajeti hiyo kwa mwaka ujao wa Fedha, Halmashauri imeambatisha maombi maalum kwa sirikali kuu ambayo ni pamoja ombi la shilingi Sh. 550,000,000 kwa ajili ya ukarati wa shule  ya Malangali ikiwa ni miongoni mwa shule kongwe hapa nchini ambazo viongozi wengi wa Taifa hili walipata kusoma Sanjari na ombi  la kupatiwa magari matatu yenye thamani ya Sh.540,000,000 maalum kwa ajili kusafirishia wagonjwa ambayo yatasambazwa katika vituo vitatu vya afya vilivyopo tarafa za Sadani, Ifwagi na Kasanga.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More