Friday, February 26, 2016

Cosato Chumi akutana na changamoto nyingi wakati wa ziara yake kwenye Taasisi za Umma na Binafsi



Mkurugenzi mkuu wa Green Resources ambao ni kampuni tanzu ya sao hill industry akifafanua jambo kwa cosato chumi mbunge wa mafinga mjini wa pili kulia, Denis kutemile anayefuatia na Hezron Vuhahula ambaye ni katibu wa mbunge


 
 Aloyce mbisha meneja mipango akimuelekeza jambo cosato chumi wapili kushoto Wakati wa ziara ya kikazi kwenye kiwanda cha sao hill mafinga. Kulia ni Denis kutemile diwani wa kata ya sao hill na kushoto ni Hezron Vuhahula katibu wa mbunge


 Vijana katika kiwanda cha sao hill wakipanga mbao baada kutoka kwenye mashine ya kichabi


 baadhi ya nguzo zikiwatayari kusafirishwa maeneo tofauti tofaiti



Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amefanya ziara katika Taasisi za Umma na Binafsi, kama Sao Hill Industries, Sao Hill Forest, Kiwanda cha Pareto na kampuni ya simu ya TTCL, Polisi, PCCB, NSSF na Bank za Mucoba, NMB,CEDB, magereza na atamalizia katika taasisi za elimu.

Akizungumza na blog hii Chumi alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha katika maeneo hayo pamoja na kujua changamoto gani wanazokumbana nazo wakati wa utendaji kazi wao.

“Nataka mafinga iwe ya kipekee kwa kuitengenezea mikakati maalumu ya kuleta maendleo ya haraka na kuwa mipango endelevu yenye faida kwa wananchi wangu unajua hili jimbo ni jimpya hivyo linachangamoto nyingi”.alisema chumi

Aidha Chumi ametembelea baadhi ya viwanda ambavyo vipo katika jimbo la mafinga na kujionea changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watendaji wa viwanda hivyo pamoja changamoto za uendeshaji wa viwanda hivyo.

“Nilipo fika katika kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini ya Kampuni ya Pyrethrum Company of Tanzania (PCT) nimekutana na changamoto kubwa ya umeme ambayo inawakwamisha katika zoezi zima la uzalishaji mali kutoka kiwanda hicho cha pareto”.alisema chumi

Chumi ameendelea kusema kuwa tatizo la umeme limeonekana kuwa kubwa kutokana na viwanda vyote alivyotembea kumlalamikia tatizo hilo na kumuomba awasaidie kulitafutia ufumbuzi ili kuongeza uzalishaji wa mali na  kuongeza pato la mji wa mafinga.

 “Nitalifaatilia na kujua nini tatizo ili tuweze kulitatua na kuwafanya mzalishe kwa wingi na muongeze ajira kwa wananchi wazao”.alisema chumi

Naye Kaimu Meneja Mkuu William Kufakwepasi wa kiwanda cha Pareto ambacho kiko chini ya Kampuni ya Pyrethrum Company of Tanzania (PCT) amesema kuwa wamekuwa wakiwalipa mishahara wafanyakazi bila kufanya kazi kutokana na tatizo la umeme hivyo wamekuwa wakipata hasara kubwa,na kumuomba mbunge wa jimbo hilo la mafinga mjini cosato chumi kuwasaidia kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo Bi Roselyne Mariki wa Green Resources (sao Hill Industries), wanaomba kuwepo Sub Station ya Umeme kwa sababu wanachukulia Umeme unaotoka Mgololo na ule wa kutoka Mafinga umekuwa unapungua sana nguvu na kupoteza asilimia 30% ya muda wa kufanya kazi kutokana na kukatika kwa umeme lakini wafanyakazi wanaendelea kulipwa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More