Thursday, January 7, 2016

VYOMBO VYA HABARI VYATUMIKA KUTATUA MGOGORO WA DALADALA MANISPAA YA IRINGA


Makamu mwenyekiti wa chama  cha daladala  mjini Iringa Best Nazaleno akifanya mahojiano  juu ya mgomo  huo  leo 
Mgogolo wa daladala manispaa ya iringa umeingia kwenye hatua nyingine baada ya viongozi mbalimbali kutumia vyombo vya habari kutatua mgogoro huo.

Akizungumza na blog hii naibu meya joseph lyata amesema kuwa wametoa taarifa kwenye vyombo vya habari ili waweze kuitwa na viongozi wa juu wa mkoa .

“Jana na juzi tumetoa kauli ikaenda redio zote za hapa manispaa kwa lengo la kuangalia kuwa je viongozi wataelewa na kututafuta hivyo tunatumia vyombo vya  habari kuwafikishia ujembena kangalia je viongozi wamesikia”.alisema lyata

Aidha lyata amesema kuwa haiwezekani mkuu wa mkoa akatawala kama rais wa mkoa huu wakati manispaa ya iringa  inaongozwa na chama cha demokrasia na maendeleo( chadema) hivyo wanamamlaka ya kuujenga mji wanavyotaka wao.
“Mkuu wa mkoa  anatumia vyombo vya ulinzi kama vyake na anavyotaka  hivyo tutaamua cha kufanya kwa kuwa hatupo tayari kuburuzwa na mtu mmoja” .alisema lyata

Lakini walipanga kufanya mgomo katika maeneo ya mshindo na miomboni lakini mapema leo asubuhi walienda kujificha maeneo ya mshindo  tu huku wakiwa wamesimama vikundi vikundi katika duka moja la mfanyabiasha.

“Hatujajificha hapa tunapita tu kwa kuwa hili eneo tunapanga mipango yetu tu na kusikiliza vyombo vya habari kwa pamoja vinasemaje na je viongozi wa mkoa watatutafuta angalia simu ya RTO inaingia ngioja nipokee nimsikilize”.alisema lyata

Lyata amesema kuwa walifuatwa na viongozi wa madereva kuwasaidia ili kutatua mgogoro huo ambao wanaona kuwa hauna maslai kwa madereva na wananchi waliowaweka madarakani.

Habari hii itaendelea hivi pundeeeeeeeeeeee

1 comments:

sebastian said...

Safi Sana lakini wimbo wangu ni ule ule pitia Habari na ubalance umesema kuwa alipokea simu ya rto je waltzingumza nini, na je waandishi wa Habari wamesaidiaje zaidi ya kulipoti tuu, mamlaka husika yaani vyombo vya dola vina simama wapi katika hili

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More