Sunday, January 17, 2016

Wahamiaji haramu themanini na tatu (83) wakamatwa mkoani iringa

  kamanda wa polisi mkoni iringa ACP PETER KAKAMBA akiwa na wahamiaji haramu kutoka ethiopia

hawa ndio  wahamiaji haramu kutoka ethiopia
 hili ndio lori lililokuwa limewabeba wahamiaji haramu kutoka ethiopia
Kamanda wa polisi mkoni iringa ACP PETER KAKAMBAakiondoka eneo la tukio

 Jeshi la polisi mkoani iringa limewakamata  wahamiaji haramu themanini na tatu(83) na watanzania wawili wakati wa dolia iliyofanyika tarehe kumi na sita mwezi wa kwanza katika kijiji cha mahenge kata mazombe tarafa ya mahenge wilayani kilolo.



Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoni iringa ACP PETER KAKAMBA amesema kuwa kuwa askari walikuwa doli walifanikiwa kulikamata gari namba T.478 DFE ambalo lilikuwa limebeba wahamiaji haramu.

Aidha kamanda KAKAMBA amesema kuwa wahamiaji haramu wamekuwa wakiipa hasara kubwa serikali kwa kuwa hudumia maradhi na vitu vingine vya kibinadamu.

Kamanda KAKAMBA amemalizia kwa kutoa onyo kwa mawakala wanaotumika kuwasafirisha wahamiaji haramu kuwa wataendelea kufanya dolia za mara kwa mara ili kudhibiti tatizo hilo na kufanikiwa kulimaliza kabisa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More