Thursday, January 28, 2016

IDARA YA KILIMO MKOANI IRINGA YAINGIA LAWAMANI


 HAPA MWANDISHI WA HABARI KUTOKA NURU FM GERLAD MALEKELA AKIWA NA MFUGAJI DR MSEKWA KATIKA ENEO LAKE LA UFUGAJI


 MFUGAJI DR MSEKWA AKIMUONYESHA MWANDISHI WA HABARI KUTOKA NURU FM GERLAD MALEKELA OFISI YA KILIMO ILIYOPO KATIKA ENEO LA UFUGAJI
 DR MSEKWA AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NURU FM GERLAD MALEKELA NA DENIS NYALI ENEO LA KUNYWESHA MAJI MIFUGO YAKE

NA FREDY MGUNDA,IRINGA

Idara ya kilimo mkoani iringa imeshauriwa kuwatembea wakulima wadogo wadogo ili kujua maendeleo yao na kutoa ushauri wa kilimo bora.

Akizungumza na blog hii Dr msekwa ambaye ni mganga wa tiba asili na mtafiti wa kilimo na ufugaji katika kijiji cha tanangozi wilaya ya iringa amesema yeye pamoja na mkewe waliweza kuusaidia mkoa wa iringa kushika nafasi ya kwanza  kwenye maadhimisho ya nane yaliyofanyika mkoani mbeya  na kupata zawadi ya shilingi milioni mbili kama wafugaji bora wa kuku wa kienyeji.

Dr msekwa anasema alitarajia viongozi na wataalamu wangemtembelea ili kumtia moyo na kumpa njia nyingine za uzalishaji bora wa kilimo na ufugaji.

 Lakini hali imekuwa tofauti toka amepata ushindi huo hajawahi kupata ushauri wowote wa kilimo kutoka idara yoyote ya kilimo wala mtaalam yeyote Yule aliyewahi kufika katika eneo analofanyia shughuri  za kilimo na ufugaji.

Dr msekwa ni mganga wa tiba za asili, mkulima ,na  mfugaji anayeishi katika kijiji cha tanangozi wilaya ya iringa amekuwa akijishughurisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji,ng’ombe wa maziwa na kuku wa mayai pamoja kilimo cha nyanya,mahindi,maharage na mazao mengine yote ya kilimo.

DR huyu ambaye pia ni Mkulima amekuwa na msaada mkubwa kwa wananchi wanaomzunguka kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kilmo pamoja na ushauri mbalimbali juu ya kilimo kwa kuwa anataaluma ya kilimo.

Aidha anasikitishwa na idara ya kilimo mkoani iringa kwa kutowatembelea wakulima wadogo kwa kuwa mara nyingi ndio wamekuwa msaada mkubwa wa mkoa katika sherehe na mazimisho mbalimbali ya kitaifa.

“Tulishinda zawadi ya shilingi milioni mbili kwa kushika nafasi ya kwanza na kuupa heshima mkoa wa iringa lakini viongozi wamekuwa hawaudhamini mchango wetu” alisema dr msekwa.

Dr msekwa amemalizia kwa kuwaomba viongozi wa mkao wa iringa wanaohusika na masuala ya kilimo kutenga muda na kuwatembelea wakulima ili kubadilishana mawazo na kuwapa ushauri wa kitaalamu na kugeuza kilimo kuwa biashara.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More