Tuesday, January 19, 2016

mwanahabari mathias canal ambatiza mtoto wake katika kanisa la kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT Usharika wa kanisa kuu-Iringa


 mchungaji wa usharika wa KKKT Iringa Brayson Mbogo akiwa na familiya ya mathias canal na Baba na Mama wa Ubatizo wa mtoto Leah Mathias Canal

 mwahabari mathiasi canal akiwa nje ya kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT Usharika wa kanisa kuu-Iringa akiwa na baadhi ya wadau pamoja na familia yake baada ya ubatizo wa mtoto wake  Leah Mathias Canal
 mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kaselela

Nianze kwa kutambua uwezo na umuhimu wa mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kaselela kwa kuhudhuria ibada ya leo kwenye ubatizo wa Mwanangu Leah Mathias Canal.

Mheshimiwa Kaselela ndiye aliyekuwa muhubiri leo katika kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania KKKT Usharika wa kanisa kuu-Iringa amesema "Ni bora kuamini katika Bwana kuliko kuamini katika mwanadamu Zaburi 118:8" 

Kwa wakristo wote ulimwenguni wanatambua kuwa leo ni Jumapili ya mwisho katika Majira ya ufunuo, kwa mkuu huyo wa Wilaya imekuwa njia pekee ya kufikisha ujumbe kwa jamii kwenye somo la utoaji kuwa baraka za mungu unaweza kuzipata kwa njia ya Utoaji hususani kwa watu wasiojiweza ama wenye matatizo kiuchumi katika jamii.

Lakini natambua umuhimu wangu nikiwa Iringa katika mahusiano baina yangu na watumishi wa mungu hususani Dkt O. Mdegela Askofu sawia na mchungaji wa usharika wa KKKT Iringa Brayson Mbogo.

Pia nawashukuru wafanyakazi wenzangu niliofanya nao kazi Ebony Fm, Nuru Fm (IDYDC) , Kwanza Jamii Ikolo Investiment Ltd), Furaha Fm, Hope Fm na wengine niliojumuika nao.

Lakini pia namshuku sana Familia ya Bwana na Bi Luckson D Luswema kwa kukubali kuwa Baba na Mama wa Ubatizo kwa Mwanangu Leah.

Lakini shukrani za dhati sana kwa Mungu maana kipekee ndiye amenipa uwezo wa kufikiri na kuona umuhimu wa imani.

"Nakubatiza Leah Mathias Canal katika jina la Baba na la wana na la Roho Mtakatifu.Amen" Alisikika Mchungaji akinena.

Naam, Ubatizo ni imani

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More