Thursday, January 28, 2016

GARI YA MAGAZETI YA MWANANCHI YAKAMATWA NA WASOMALI



NA RAYMOND MINJA IRINGA.

Jeshi la  Polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Jeshi la uhamiaji lilinawashikiria  watu 11katia yao wahamiaji haramu 8 raia wa Ephiopia kwa kuingia nchini bila kibali.

 Katika tukio hilo watanzania watatu wakiwamo dereva na msaidizi wake wa gari la kukodi linalotumika kusafirisha magazeti yanayochapishwa na kampuni ya  Mwananchi Communications Ltd na mtu mmoja liyejitambulisha kuw a ni msindikizaji wanashilikiwa na jeshi hilo  kwa kushiriki kusafirishwa watuhumiwa hao.

Akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa jana Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Peter Kakamba alisema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye kituo cha ukaguzi cha Polisi cha Igumbilo.

“Ndugu zangu leo (jana) majira ya saa 11 alfajiri katika eneo la kizuizi cha Polisi cha ukaguzi wa magari Igumbilo (Chek Point) ndani ya Manispaa ya Iringa,Polisi katika ukaguzi wa kukagua magari walilikamata gari hiyo aina ya Toyota Hiace yenye namba za usaliji T.745 DED.likiwa limepakia magazeti ya Mwananchi na wahamiaji kutoka Ephiopia 8”alisema Kakamba

Aliwataja madeva waliokuwa wakiendesha gari hilo kuwa ni Godfrey Kaka 32)akiwa na masaidizi wake Michael Jafet (37) wote wakazi wa Jijini Dar es Salaam na mtu mmoja aliyefahamika kwa Elias Patson mkazi wa Jijini Dar es Salaam aliyedai alikuwa msindikizaji.

“Bado haijafamika kama huyu aliyejitambulisha kuwa ni msindikizaji alikuwa asindikiza wahamiaji haramu ama magazeti na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi juu ya jambo hili”alisema Kakamba.

Kakamba alifafanua kuwa mara jeshi litakapomaliza kazi ya uchunguzi na kwa kushirikiana na jeshi la uhamiaji watawafikisha watuhumiwa hao mahakamani kujibu shitaka lao.

Alionya kuwa oparesheni ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu yakiwamo makosa mbalimbali pamoja na wahamiaji haramu itaendelea hadi hapo watakapohakikisha vitendo hivyo havijirudii.

Naye Mmoja wa watuhumiwa hao ambaye ni dereva wa gari lililotumika kusafirisha magazeti hayo  Michael Jafet alisema waliwapakia wahamaiaji hao eneo la Mbezi jijini Dar es Salaam.

“Sisi tulipokuwa tukiondoka jana majira ya saa nane usiku kwenye makoa makuu ya Ofisi za Mwananchi Communications Ltd na tulipofika eneo la Mbezi mtu mmoja ambaye hatumfahamu alisimamisha gari na kutuomba tuwapakie watu hawa akitutaka tuwashushe eneo la Nyololo mkoani hapa”alisema Jafet.

Alifafanua kuwa kila mtu katia yahao walioapanda waliwalipa Sh 30,000 kama nauli ya kutoka Dar es Salaam hadi Nyololo mkoani Iringa.

Tukio hilo limekuja wakati kasi ya kukamatwa kwa watuhumiwa wanaoingia nchini kinyume na sheria ikizidi kuongezeka kila uchao.

Januari 16 mwaka huu katika eneo la Mahenge kata ya Mazombe wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa Polisi walikamata watuhumiwa 85 kati yao wahamiaji haramu kutoka Ephiopia wakiwa 83,na jana watuhumiwa 11 raia kutoka Ephiopia wakiwa nane.

Hatua hiyo imefanya jeshi la Polisi Mkoani Iringa kuwashikilia watu walioingia nchini kinyume na sheria kufikia 91katika kipindi cha mwezi januaria pekee.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More