Sunday, January 17, 2016

Wanajeshi waliojeruhiwa na Alshabaab wawasili

  Wanajeshi wa Kenya waliojeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na wapiganaji wa al shabaab katika eneo la el adde wamesafirishwa hadi Nairobi.
Wapiganaji hao wa Al shabaab walishambulia kambi ya jeshi la umoja wa mataifa nchini Somalia na kuna ripoti kuwa wanajeshi kadhaa wa Kenya waliuawa huku wengine wakijeruhiwa.

Idadi ya wanajeshi waliouawa haijabainika wazi lakini kundi hilo la Al shabaab linadai kuwa liliwauwa zaidi ya wanajeshi sitini madai ambayo serikali ya Kenya imekanusha.

Aidha amesema wanajeshi wa Kenya bado wangali wanapambana na wapiganaji hao wa Al shabaab ili kujaribu kuwakomboa wanajeshi waliokwama ikiwa wapo.
Kenya imekariri kuwa haitaondoa wanajeshi wake Somalia hadi pale kundi hilo la al shabaab litakaposambaratishwa kabisa na amani kurejea nchini humo.

Wakati huo huo kundi hilo limedai kuwa linawashikilia wanajeshi kadhaa wa Kenya mateka.

Al Shabaab limesema ni mara ya kwanza kikosi chake maalum cha Saleh ali saleh Nabhan kilifanya shambulio ndani ya somalia.
Saleh ali Saleh Nabhan alikuwa kiongozia wa Al qaeda katika kanda ya Afrika mashariki na aliuawa kwenye shambulio lililofanywa na Marekani mwaka wa 2008

Tangu mwaka wa 2011 wakati Kenya ilituma wanajeshi wake nchini Somalia, kundi hilo limefanya mashambulio kadhaa ya kigaidi nchini Kenya na kusababisha maafa makubw

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More