Mratibu
wa mradi wa SPANEST na mwenyekiti wa SPANEST Band Godwell Ole Meing’ataki akiwa katika maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
SPANEST Band wakitumbuiza wakati wa maonyesho ya utalii wa kanda ya nyanda za juu kusini yalifanyikia katika mkoa wa Iringa viwanja vya kanisa la kikatoliki la parokia ya kihesa maarufu kama uwanja wa kichangani.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
SPANEST Band ya mkoani Iringa yaendelea kutoa
elimu ya utalii na kupiga vita ujangili kwa watanzania kupitia nyimbo
mbalimbali ambazo zimekuwa zikihamasisha wananchi kuujua utalii,kutunza vivutio
vyote vya kitalii na kuacha kuuwa wanyama wanaoendelea kuliingizia taifa pato kupitia
utalii.
Akizungumza na blog hii mratibu
wa mradi wa SPANEST na mwenyekiti wa SPANEST Band Godwell Ole Meing’ataki alisema kuwa
wameamua kuanzisha Band hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya utalii na kupiga vita
ujangili kwa njia ya sanaa ili kuwafiki wananchi walio wengi.
“Unajua kuwa watu wengi
wanapenda kusikiliza nyimbo na kuona maenyesho ya wasanii hivyo uwepo wa
SPANEST Band umesaidia kutoa elimu ya utalii ndio maana unaona kwenye maonyesho
mengi wakuwa wakitumbuiza na kupendwa na kila mtu anayekuwa katika eneo hilo”
alisema Meing’ataki.
Meing’ataki alisema kuwa nyimbo za SPANEST Band
zinatoa elimu mahususi ya maswala ya utalii hivyo imekuwa kazi rahisi kuwafika
vijana na watu wengine wa rika mbalimbali ambao wamekuwa wakihudhuria matamasha
au maonyesho ya kitalii.
Aidha Meing’ataki alisema
kuwa Band hiyo tayari imeshasajili na baraza la Sanaa na michezo (BASATA) hapa
nchi ili kupata fursa ya kutumbuiza katika maonyesho yoyote hapa nchini na
kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa watanzania na wasio watanzania.
“Usiposajili kazi yako
utakuwa unajinyima haki yako ya msingi hivyo band hii ya SPANEST imesajili na
BASATA wanaijua hivyo kuifanya kufanya hata kazi za serikali kwa kuwa waandaa
nyimbo zao bila kukiuka sheria za nchi” alisema Meing’ataki
Meing’ataki aliwaomba wadau
mbalimbali wa utalii na uhifadhi kuendelea kuiunga mkono SPANEST Band ili
wapate nafasi ya kuendelea kutoa elimu kwa njia ya Sanaa ya uimbaji ambao kwa
kiasi kikubwa kwa sasa vijana wengi wanaitumia.
“Mimi nawapongeza sana
wasnii wote wa SPANEST Band kwa kazi wanaifanya kuelimisha jamii kwani
wanatunga nyimbo zao vizuri na zinahamasisha wananchi kupembela vivutio vyao na
kupiga vita ujangili wa wanayama ambao ndio vituo vikubwa kwenye mbuga zetu
hapa nchini” alisema Meing’ataki
Naye katibu wa band hiyo Denis
Nyali alisema waliamua kuanza kuandaa nyimbo za kuhamasisha utalii na kuacha
kuuwa wanyama kutoka na kufanya utalii katika mbuga mbalimbali na kijionea vitu
vingi ya kuvutia.
“Mimi ni mwandishi wa habari
hapa mkoani Iringa tulikuwa tumeenda kutalii katika mbuga ya Ruaha iliyopo
mkoani Iringa tukapewa zoezi la kutafuta njia za kutoa elimu ya kupinga
ujangili na kutoa elimu ya utalii na ndio ulikuwa mwanzo wa kuanzisha SPANET Band”
alisema Nyali
Nyali alimpongeza mratibu wa
mradi wa SPANEST Godwell Ole Meing’ataki ambaye
pia ni mwenyekiti wa Band hiyo kwa juhudi zake za kuanzisha na kuendeleza kwa
kuwaongezea majukumu ya kutumbuiza kwenye matasha mbalimbali ya utalii na kuzifanya
nyimbo zake kuwa maarufu.
“Unajua sisi ni wasanii tu
hivyo bila kuwa na mtu anayetusaidia hatuwezi kufika popote pale ndio maana
kushikwa mkono na mratibu wa mradi wa SPANEST Ole Meng’ataki kumetusaidia
kuendelea kutunga nyimbo na kufanya video za nyimbo hizo ambazo zimekuwa na
mvuto kwa jamii” alisema Nyali
Nyali alisema kuwa lengo la
Band hiyo ni kuendelea kutoa elimu ya kitalii kwa kutumia nyimbo ambazo wanazoziimba
kwa njia tofauti tofauti kufikisha ujumbe halisi kwa wanachi waupende utalii na
kupiga vita ujangili ambao umekuwa ukirudisha nyuma maendeleo ya utalii.
“Tunawaomba wananchi wawe na
subila hivi karibuni tutawaambia kuwa nyimbo hizi zitapatikana wapi kwa kuwa
Band hii ipo chini ya mratibu wa mradi wa SPANEST hivyo tunasubili muungozo wa
kutoka kwao kwa kuwa kazi yetu tumeshamaliza ya kurekodi na tunaendelea
kutumbuiza katika maonyesho mbalimbali ambayo tunakuwa tunaalikwa” alisema
Nyali
0 comments:
Post a Comment