Monday, October 2, 2017

DC MTATURU AWATAKA WANANCHI KUHIFADHI FEDHA ZAO BENKI

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja.
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito akizungumza jambo mara baada ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikata keki ishara ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi, Mkoani Singida.
Shilinde Kurwa Kasule ambaye ni mfanyabiashara akielezea namna alivyonufaika kwa kupata mikopo mbalimbali kutokana na utunzaji wa fedha zake Benki.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Mwenye Shati la kitenge), Kushoto kwake ni Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Winfrida Funto wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi wakiongozwa na
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kulia) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Benki hiyo mara baada ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi.

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewataka wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyingi majumbani na badala yake wajenge utamaduni wa kuzipeleka benki ili kuepusha kuhatarisha usalama wao. 

Ametoa kauli hiyo leo Octoba 2, 2017 wakati akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo Wilayani humo Mkoani Singida.

Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha majumbani si nzuri kwa sababu wanahatarisha usalama wao, hivyo ni vyema wakatumia benki hiyo iliyoanzishwa hivi karibuni kwa ajili ya kutunza fedha zao.

Alisema mbali ya kuhatarisha usalama kwa utunzaji wa fedha ndani ya nyumba pia kuhifadhia fedha nyingi ndani Ni kosa kisheria kwani kunasababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo Jambo ambalo linafifihisha ukuaji wa uchumi.

Katika hatua nyingine Mhe Mtaturu aliupongeza uongozi wa benki ya NMB kwa kutii maoni ya waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa Desemba 5, 2016 wakati akifungua tawi la benki ya Biashara ya Uchumi lililopo wilayani Karatu mkoani Arusha la kupunguza kiasi cha riba wanachokitoza katika mikopo wanayoitoa ili kuwawezesha wananchi kukopa na kupata tija.

Alisema kuwa kuanzishwa kwa NMB CHAPCHAP INSTANT ACCOUNT na kupatikana kwa riba ya mpaka asilimia tano kwa wateja Ni kichocheo Cha muelekeo wa wananchi kupata Huduma laini katika Benki hiyo ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.

Sambamba na hayo pia Mhe Mtaturu aliushauri Uongozi wa Benki hiyo kufanya Utafiti katika maeneo ya Wilaya nzima ili kuwa na namna Bora ya kuwafikia wateja wote ambao bado hawajaanza kunufaika na Huduma hiyo na Huduma za kibenki ikiwemo uhifadhi wa fedha Hizo.

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito alisema kuwa wiki ya Huduma kwa mteja inawarahisishia wateja kutoa maoni yao ili kuwa na namna Bora ya kuboresha Huduma katika Benki hiyo.

Alisema kuwa Benki hiyo imeanzisha Huduma ya Akaunti ya CHAP CHAP ambayo itamuwezesha mteja kupata Huduma za kibenki na Haina kima Cha chini Cha salio kwenye Akaunti Wala makato ya mwezi.

Aliongeza kuwa NMB CHAP CHAP Akaunti Ni Huduma Bora na nafuu inayomuwezesha mteja kufanya shughuli zake zote za kibenki papo kwa papo bill shida popote alipo kwa kutumia Simu ya mkononi kupitia Huduma ya NMB Mobile.

Naye Shilinde Kurwa Kasule ambaye ni mfanyabiashara na mtumiaji mkubwa wa Huduma za Benki ya NMB aliwasihi wananchi na wafanyabishara Wilayani Ikungi kutohifadhi fedha ndani badala yake wahifadhi Benki kwa ajili ya usalama wao na fedha zao.

Shilinde alisema kuwa kuweka fedha benki Ni njia mojawapo ya wananchi na wafanyabishara kuiaminisha Benki kuwa wanakopesheka kwani watakuwa wanajua mzunguko wa biashara ya mteja wao.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More