Rais John Magufuli amewatoa hofu wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuhusu
uteuzi wao kwa kuwataka kuchapa kazi kwa bidii ili wawe na nafasi nzuri
ya kuteuliwa badala ya kufanya kazi kwa wasiwasi jambo ambalo matokeo
yake yatakuwa kuondolewa.
Hatimaye
wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa
linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa
husika.
Binti
mmoja anayejulikana kwa jina la Jesca ambaye ni mfanyakazi wa Longido
Mountain Lodge amekutwa amejinyonga katika hotel ya Longido Mountain
Lodge na kuacha ujumbe kuwa kifo chake kisihusishwe na mtu yeyote
Watu
wawili wameuawa mkoani Shinyanga katika matukio mawili tofauti,
likiwamo la kijana kuchomwa kisu akigombea mwanamke katika baa ya Matunu
mjini Shinyanga.
Watu wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
wakikabiliwa na tuhuma za kujipatia fedha kwa kutumia jina la Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa.
Wafanyakazi watatu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoani Morogoro,
wanashikiliwa na Polisi wakihojiwa kutokana na kifo cha mfanyakazi
mwenzao, Deo Elias (30), mkazi wa Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kwa
kunaswa na umeme juu ya nguzo.
Kufuatia
tukio la ndugu wa mgonjwa kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi
la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha
kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Msanii Emmanuel Simwinga maarufu “ Izzo Bizness “ akitumbuiza
kwenye tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya
jumapili iliyopita.
Askofu wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhu kabla ya kuliombea taifa lipate mvua akiwa na wachungaji mbalimbali. Kulia ni Mchungaji Palemo Masawe.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Banakunu (kulia), wakitembea wakati kamati hiyo ilipotembelea MSD Makao Makuu Keko Dar es Salaam.
mbunge wa jimbo la Mafinga
mjini mkoani Iringa Cosato Chumi akiwa na balozi wa
korea mh Geum-young song wakipata picha ya pamoja baada ya maongezi ya muda mrefu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe,
amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi
yaliyopinduliwa; na kwamba matokeo hayo yawe chachu ya kufanya vizuri
zaidi katika uchaguzi ujao.
Serikali
za Tanzania na Uganda zinatarajia kuanzisha mradi wa uwekezaji wa
ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta unaolenga kuongeza pato la taifa na
uchumi wa nchi hizo.
Utafiti
uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na upimaji
wa virusi vya Ukimwi la MATUMAINI, unaonyesha kuwa kati ya wanawake kumi
wanaofanya biashara ya ngono wanaopima wanne kati yao wanakutwa na
virusi vya Ukimwi.
Askari polisi na wasamaria wema
wakisaidia kutoa maiti kutoka katika basi la Lupondije Express namba T
798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya kupinduka eneo la Mteremko wa
Ipogolo mjini Iringa.
Polisi mkoani Ruvuma inawashikilia waendesha bodaboda 20 Manispaa ya
Songea wanaodaiwa kumshambulia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) Kikosi cha 411 KJ Ruhuwiko, kwa kupiga mawe gari alilokuwa
akiendesha baada ya kumgonga mtembea kwa miguu.
Askari polisi na wasamaria wema
wakisaidia kutoa maiti kutoka katika basi la Lupondije Express namba T
798 AKV kutoka Mwanza - Iringa baada ya kupinduka eneo la Mteremko wa
Ipogolo mjini Iringa.
WATU
saba wamekufa na wengine 10 k u j e r u h i w a baada ya gari
walilokuwa wanasafiri nalo aina ya Mitsubishi Fuso kupasuka tairi la
mbele na kugonga kingo za barabara katika barabara kuu ya
Igunga-Singida.
Mtoto
wa siku moja ameibwa katika mazingira ya kutatanisha katika Hospitali
ya Rufaa ya Bugando, akiwa pembeni mwa mama yake aliyekuwa amelala,
mwenye umri wa miaka 16.
Madereva watatu wa malori yaendayo mikoani na wasaidizi wao watatu,
wamenusurika kifo baada ya kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwilini
na mlinzi wa nyumba moja ya wageni iliyopo Ubena, Chalinze mkoani Pwani.
Siku
chache baada ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuapishwa baada
ya kushinda uchaguzi wa marudio uliosusiwa na baadhi ya vyama vya
upinzani, Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif
Hamad, amerejea Zanzibar.
Polisi mmoja anadaiwa kumpiga risasi dereva daladala, Pistus Ngowi baada ya kutofautiana kauli.
Tukio
hilo lililotokea juzi saa tatu usiku, Kariakoo jijini Dar es Sallam
lilisababisha madereva wenzake wanaofanya wote safari za Tandika pamoja
na wa Temeke kugoma kwa zaidi ya saa tano wakidai kwamba licha ya
kushambuliwa, amebambikiwa kesi katika Kituo cha Polisi cha Msimbazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe ameagiza mamlaka zinazohusika
kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu watakaobainika
kutafuna fedha za mishahara hewa kabla ya mwezi huu kumalizika.
Serikali imeunda kikosi kazi kinachohusisha taasisi nyeti nchini
kuchunguza sakata la kukamatwa kwa raia wawili wa Uholanzi wakiwa katika
harakati za kusafirisha tumbili 61 kwenda nchini Albania.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, SACP Justus Mamugisha, akitoa taarifa kwa wanahabari.
Watu
wawili wameuawa Jijini Mwanza kwa kupigwa risasi na Majambazi, huku Wengine
saba wakijeruhiwa katika tukio la uvamizi wa duka lililokuwa likitoa huduma mbalimbali
za kifedha. Habari Zaidi BONYEZA HAPA.
Siku
tatu baada ya kuibuka kwa kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) imemuita Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kumhoji.
Muda
mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa
Nzega Mjini, Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya Huduma za
Jamii, walimuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye
nafasi zao ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
KAMATI
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeshindwa kujadili Deni
la Taifa na kuagiza kukutana na idara na taasisi sita, zinazohusika na
deni hilo.
Jeshi
la polisi mkoani Arusha jana lilifanikiwa kumnusuru meneja wa kiwanda
cha kutengeneza bidha za plastiki cha Best Pack kilichopo jijini
Arusha,Vijay Kumar raia wa India baada ya kunusurika kupigwa na baadhi
ya wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhura wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza.
Siku
mbili baada ya baadhi ya wabunge kudaiwa kuhusika katika vitendo vya
rushwa, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa
(Takukuru), Valentino Mlowola amesema taasisi yake inawahoji wote
waliotajwa kuhusika na tuhuma hizo.
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kutoa lugha
chafu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda inayomkabili
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, Aprili 13, mwaka huu.
Walinzi
watatu wa Suma JKT na askari mmoja wa Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa
Dodoma, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta zinazokadiriwa
kufikia 50 mali ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom).
Ujumbe
wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) umeridhishwa na juhudi
zinazofanywa na Serikali ya Rais John Magufuli katika kuongeza juhudi za
kupambana na rushwa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akizindua rasmi ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Bi. Eda Sanga akifungua mkutano huo wa siku moja jinsi ya kutoa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia unaosababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi
Msichana
wa umri wa miaka 17 ambaye alikuwa katika machungu ya uzazi, amejikuta
akijifungulia mtoto chooni baada ya muuguzi mmoja wa Hospitali ya Amana
jijini Dar es Salaam kumtaka aende kuoga na kubadilisha nguo bila ya
kujali hali yake.
Hatimaye
kitendawili cha watu watatu walionyongwa kisha kuchomwa moto kwenye
Gesti ya Mexico mjini Kyela, kimetenguliwa baada ya ndugu kujitokeza na
kuwataja kwa majina halisi.
SIKU
mbili tangu kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Zanzibar, na siku moja
kabla ya kuapishwa Dk Ali Mohamed Shein, Maalim Seif Shariff Hamad,
Mgombea wa Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana
kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amesema CUF haitashiriki uchaguzi
wowote chini ya Tume ya Jecha Salim Jecha.
Jeshi
la Polisi jana walitumia mabomu ya machozi kurejesha hali ya amani
baada ya wananchi kuanza kupigana kwa sababu za kisiasa wakati
wakisherehekea ushindi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein,
katika kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni, Pemba.
Hatimaye uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es Salaam umekamilika leo katika ukumbi wa Karimjee, na kushuhudia Isaya Mwita wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameishtumu
Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe
wammepokea rushwa.
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL)
na DW, Salma Said amedai alitekwa na wanaume wawili baada ya kumkamata
na kumuingiza kwenye gari lao kisha kuondoka naye na kumpeleka
kusikojulikana.
AWakati
Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi
hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya
Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli
asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati
wowote.
Naibu Spika wa Bunge, Tulia Mwansasu (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo alipohudhuria kikao cha kamati hiyo kilichoketi katika Kumbi za Benki Kuu (BoT Dar es Salaam leo.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, William Ngeleja.
Idadi ya waliokufa kutokana na ugonjwa wa
kipindupindu katika tarafa ya Pawaga, wilaya ya Iringa mkoani Iringa imeongezeka na kufikia watano
baada ya mgonjwa wengine kufariki na kuzikwa jana kijiji cha Luganga.
Aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif
Sharif Hamad ambaye alitangaza kususia uchaguzi wa marudio licha ya jina
lake kujumuishwa kwenye makaratasi ya kura, amesema ameiachia CCM
kuamua hatma ya nchi hiyo.