Monday, May 21, 2018

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI 40 MKOANI IRINGA KUANZIA TAREHE 23 / 05 /2018


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru mkoani hapa kwa kufanya shughuli ya kuzindua jumla ya miradi arobaini (40) 
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakiwa wanamsikiliza mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ofisini kwa hii leo


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Jumla ya miradi 40 ya maendeleo nyenye thamani ya shilingi 24,427,360,696 inatarajiwa kuzinduliwa na mwenge wa uhuru mkoani iringa kuanzia tarehe 23 / 05 /2018 wilayani mufindi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mwenge wa uhuru utatembelea mira mbalimbali ikiwamo miradi kumi ya sekta ya elimu,afya miradi saba,maji miradi mine ,maliasili mmoja,kilimo mitano,uvuvi mmoja viwanda miwili na mapambano zidi ya rushwa mine.

“Gharama za miradi hiyo zimetokana na michango ya wananchi shilingi 1,251,610,850, serikali kuu kiasi cha shilingi 8,638,969,449.40, halmashauri  kiasi cha shilingi 253,564,461 na wadau wa maendeleo kiasi cha shilingi 14,283,215,936” alisema Masenza

Aidha Masenza aliitaja ratiba ya mbio za mwenge wa uhuru mkoani Iringa itakuwa kama ifuatavyo tarehe 23 /05 2018 mwenge wa uhuru utapokelewa halmashauri ya Mufindi,tarehe 24 / 05 / 2018, halmashauri ya wilaya ya iringa,tarehe tarehe 25 / 05 / 2018 halmashauri ya Kilolo, tarehe 26 / 05 / 2018 halmashuri ya manispaa ya iringa na tarehe 27 / 05 / 2018 na halmashauri ya mji wa Mafinga na baada ya hapo mwenge wa uhuru utaelekea mkoani Njombe kuanzia tarehe 28 / 05 / 2018.

Masenza alisema kuwa kauli mbiu ya mwaka 2018 ya mwenge wa uhuru ni elimu ni ufunguo wa maisha ;wekeza sasa kwa maendeleo ya taifa letu. Na ujumbe huo unalenga kuweka mkazo kwenye umuhimu wa uwekezaji wa elimu bora unaofanywa na serikali pamoja na wananchi wa maeneo husika.

“Serikali imeweka mikakati madhubuti ya kupinga vita umsikini na kujenga taifa lenye maendeleo ya viwanda hivyo ndio maana katika maeneo mengi hapa nchini swala la elimu limepewa kipaumbele na kuhakikisha kuwa tunapata wasomi wengi ambao watasaidia kuendesha viwanda hapa nchini” alisema Masenza

Masenza alisema kuwa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2018 zilizinduliwa mkoani Geita na mheshimiwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 2 /5 / 2018 na mwenge huu utakimbizwa kwa mikoa 31 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhitimishwa na rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mkoani tanga tarehe 14 /10 /2018

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More