Monday, January 4, 2016

KIWANGO CHA UFAULU DARASA LA 07 CHAPANDA MUFINDI


 SAADA MARUNDE mkurugenzi mtendaji wilaya ya mufindi

Na Mpoki Mwakapiso,mufindi
 
Zaidi ya wanafunzi elfu 05 miamoja wa shule za msingi Wilayani Mufindi Mkoani Iringa, wanatarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza baada ya kufaulu mtihani wa darasa la 07 ulifanyika mapema mwaka jana huku ufaulu huo ukipanda na kufikia asilimia 80.39 ukilinganisha na asilimia 68.21 ya mwaka 2014

Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya wilaya ya mufindi kwa nyombo vya habari, imetanabaisha kuwa, wanafunzi waliokuwa wamesajiliwa   kufanya mtihani walikuwa elfu 07 miambili 20 na miongoni mwao waliofaulu na kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari ni elfu 05 miamoja 98.


Taarifa hiyo imeainisha mgawavyo wa wanafunzi hao kwa kuzingatia jinsi, ambapo kati ya waliofaulu, wasichana wameongoza kwa takwimu za ufaulu huo wakiwa elfu 02 mianane 31 wakifuatiwa na wavulana elfu 02 miatatu 67. Aidha, wanafunzi wote waliofaulu wamepangiwa shule ili kuendelea na elimu ya sekondari itakayokuwa ikitolewa bure hapa nchini.


Wilaya ya Mufindi yenye jumla ya shule za msingi 178 imeshika nafasi ya pili Mkoani Iringa kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwa asilimia 80.39 ikitanguliwa na Manispaa ya Iringa iliyofaulisha kwa asilimia 80.55 ikiwa na jumla ya shule za msingi 50

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More