Serikali
imesema uamuzi wa kurudia uchaguzi wa urais Zanzibar ni halali na wa
kisheria na kwamba wanaotafuta suluhu nje ya Katiba, wanakosea.
Kauli
hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira, January Makamba alipokuwa akihitimisha majadiliano ya
kuchangia hotuba ya Rais John Magufuli.
Alisema
uchaguzi ulifutwa kisheria na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa
Tangazo la Serikali Namba 6587. Makamba alisema Katiba ya Zanzibar,
imeeleza wazi kuwa hakuna mamlaka ambayo itahoji uamuzi wa tume, hata
kama ni Mahakama. Alisema akidi ilitimia wakati tume inafikia hatua
hiyo.
Waziri huyo alisema wanaotaka kutumia suala hilo kuleta vurugu Zanzibar, damu za Watanzania zitawalilia.
Alisema viongozi wakuu wa nchi, wamefanya kazi kubwa katika kulitafutia
ufumbuzi suala hilo na hivyo ieleweke kuwa ZEC na NEC ni tume
zinazojitegemea.
Alisisitiza
NEC haiwezi kuingilia uamuzi wa ZEC, kwani uchaguzi wa rais uliofanyika
kwa siku moja Tanzania Bara na Zanzibar, umekuwa ukiendeshwa na Tume
mbili tofauti. Alisema uchaguzi huo, ulifanywa na tume tofauti na hata
wino uliotumika katika chaguzi hizo ni tofauti .
Alisema
wajibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuhakikisha kuwa amani na
utulivu, vinalindwa Zanzibar katika marudio ya uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Machi 20 mwaka huu.
Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, alitoa “Taarifa Kwa Umma ya Kufuta Uchaguzi wa Zanzibar”.
Katika taarifa hiyo, Jecha Salim Jecha alisema “Mimi
nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, nimeridhika kwamba
uchaguzi huu haukuwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na
taratibu za uchaguzi.
Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba
uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya
kurudia uchaguzi huu”.
0 comments:
Post a Comment